Ninamashaka na Masoud Djuma wa Simba SC Kuelekea Mzunguko wa Pili.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Furaha imewatanda kuondoshwa kwa Omog. Je mmewahi kuwaza ni jinsi gani huyu Kocha msaidizi Masoud Djuma ataweza kuiongoza Klabu yenu mzunguko wa pili unaokuja kuanza ukizingatia Jamaa ni mgeni kwenye Ligi Kuu ya Tanzania?

Kufukuzwa kwa Omog katika kipindi hiki cha dirisha dogo haikuwa jambo la Busara.

Ninachotegemea mimi ni kuwa Masoud Djuma atakuwa akijaribu kuinject falsafa yake kwenye timu wakati klabu inaendelea na mechi za mzunguko wa pili....Hivyo basi hii itapelekea timu yenu kuteteleka huku wachezaji wakijaribu kuenenda na falsafa ya mwalimu.

Hovyo naona Mzunguko wa pili ni karata turufu kwa Klabu ya Simba kuukosa Ubingwa rasmi.
 
Kauli yako haina ukweli
Viongozi hawakuwa na hitaji la Omog
Wachezaji hali kadhalika
 
....... labda kama uamini uwezo wa Masoud Djuma; ila atakama angeletwa Gadiola kuja kuinoa Simba naye angetakiwa kui-enject falsafa mpya. .....provided formula na kanuni za mpira zinajulikana na kama wachezaji watatambua majukumu na wajibu wao usifikilie kushindwa.
 
Mo anazo pesa kinachomshinda kusajili kocha mkuu wa Simba nn? Ukweli upo wazi kuwa makocha wachache sana ambao wamekuwa wasaidizi kupewa timu kuziongoza na kuchukua ubingwa ila wengi wao ambao ni makocha wasidizi husaidia timu iwe kwenye nafasi nzuri , wasipokuwa makini Simba, ubingwa watausikia kwa Yanga, wajipange watafute kocha mkuu waache kupenda mteremkoo kuwa bingwa kunahitaji gharama.
 
10% watu washakula,kazi kwake akizungua wanaleta mwingine watu km kawa wanakula cha juu,na uzuri sasa hv tajiri yuko ,pesa iko
 
Nimefurahia uamuzi wao. Ni faida kwa Yanga. Harafu robo ya mwisho walete kocha mwingine iwe raha zaidi kwa Yanga
 
Nimefurahia uamuzi wao. Ni faida kwa Yanga. Harafu robo ya mwisho walete kocha mwingine iwe raha zaidi kwa Yanga
Hahahaha, dah adui ndio unamuombea njaa?OK nauliza tu Huyu Masoud amepewa timu kwa malengo yapi?...atwae mapinduzi cup?, atwae vpl? atwae champions league? au timu ifunge magoli mengi ?
 
Kauli yako haina ukweli
Viongozi hawakuwa na hitaji la Omog
Wachezaji hali kadhalika
Yani usiwe na hitaji la kocha anayeongoza ligi? Shida ya viongozi wa simba ni kuwa na matarajio makubwa kila wanaposajili majina makubwa! Wanasahau kuwa mpira unachezwa uwanjani. Yan umuache ajibu umsajili niyonzima? Ni kweli simba bado inamuhitaji okwi? Wakati wenzao wanasajili wachezaji wadogo kama kina ajibu, gadiel, baswita, rafael daud nk. Wao wanajaza wakongwe ili waifunge yanga
 
Viongozi wa ajabu sana
 
Simba inawapiga dili kibao ,jiulize kila round wanaleta wachezaji wa kigeni,Ghana,ivory coast na mwingine,but wanacheza miezi 6,tu kisha tunatangaziwa wamemuacha jiulize
Agban
Agey
Blagnon
Bukungu
Mwanjali
Mavugo
Hao wote hkn sababu ya msingi ya kuachwa ila kwakua walikuja kimipango watu wapate 10%,wakawasainishi vile wanavyotaka( maelewano ukiperfome tutakuongeza) mchrzaji akishtuka anapewa zengwe

Na makocha hivyo hivyo
Simba tatizo viomgozi ni wapiga dili wengine ni wale FoS ,na wengine wanajiita Simba makini

Wanachama na Mo msiposhtuka mtaliwa daily,hapo kn genge la wezi
 
Kwani yule mikofia pop kazi yake ni ipi pale simba mbona anaonekana ana nguvu kubwa iliyojificha?
 
Kwani yule mikofia pop kazi yake ni ipi pale simba mbona anaonekana ana nguvu kubwa iliyojificha?
Anasajiri wachezaji kwa pesa zake kisha anaipiga club cha juu,usije ukawaza kuwa anasajiri kwa mapenzi NO,huwa anarudishiwagwa /wanaidai club ndio maana ana nguvu mno
 
Anasajiri wachezaji kwa pesa zake kisha anaipiga club cha juu,usije ukawaza kuwa anasajiri kwa mapenzi NO,huwa anarudishiwagwa /wanaidai club ndio maana ana nguvu mno

duh kweli kazi ipo..
 
hivi hao MAKOMANDOO wa simba wana kazi gn,,hao ndy wanaozinguwa timu pamoja na hao viongozi uchwara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…