Ninamiliki blogu inayoniingizia wastan laki 4 kila mwezi, sio pesa ya haraka bali ni uvumilivu na consistency

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Blogging sio kazi yangu, naweza kusema ni kama aina ya mti nilioupanda mimi navuna tu, nina shughuli zingine

Watu wengi wanapofungua blog wazo linalowajia, ngoja nifanye kama blogger flani niposti habari za michezo, miziki, udaku, n.k. hapa ndipo watu wengi sana wanafeli na kuzifunga blogs zao kwasababu zinakosa watembeleaji

Out of nowhere ufungue blog ya ajira ni ngumu kushindana na kina Millard ayo na magwiji wengine, utapigwa kanzu hasa ukizingatia wao wana majina tayari na wamesomea uandish wa habari na wameajiri vijana.

Bloggers wakubwa vipato vyao wanategemea matangazo, mfano blogger maarufu anapata watazamaji laki kila siku, kampuni za hapa hapa kwetu zinaweza kumuomba atangazie biashara zao kwa dau flani lets say milioni kila mwezi, ni kampuni moja tu hilo. unakuja kwa google hawa wanalipa kama dola 1 kwa kila watazamaji elfu moja ambayo ni sawa na shilingi 2,500, so matangazo yanafaa zaidi bloggers wenye watembeleaji

mimi nilianzisha blog yangu kama hobby tu, kuandika vitu ninavyovijua kwa undani, nilikuwa napata viewer kama 10 tu kwa wiki, baada ya research binafsi nikaona nijikite na kitu kimoja tu ambacho tupo bloggers wachache sana, yani blog iwe imejaa taarifa au habari za kitu flani tu mwanzo mwisho,

Kwa mfano blog iwe inazungumzia chunusi tu, unajaza posts kama
  • Vipodozi bora kwa ngozi yenye chunusi
  • Njia za kuondoa chunusi kwa haraka
  • Sababu za chunusi na jinsi ya kuzizuia
  • Vipodozi vya asili vya kutibu chunusi
kama unapenda magari unaweza kudeal zaidi na matengenezo
  • Jinsi ya kutunza gari lako ili lidumu kwa muda mrefu
  • Makosa ya kuepuka unapofanya matengenezo ya gari
  • Gharama za matengenezo ya gari Tanzania
Blogs kubwa kuna muda huwa zinachapisha hizi posti lakini tofauti ni kwamba mimi nimejikita zaidi na kitu kimoja tu na muhimu zaidi kuna blogs chache au hakuna kabisa zinazungumzia chunusi tu, kwenye matokeo ya google mdogo mdogo unaanza kupewa kipaumbele kwenye matokeo ya chunusi, magari, n.k. google wanapenda sana ukiwa una deal na kitu kimoja tu ila ponea yako competition isiwe kubwa sana, mfano ukianzisha blog ya simba au yanga cometition ni kubwa, blogs kibao zimejikita huko, nadhani mnanielewa

Muda unavyozidi kwenda nikawa naona napata watembeleaji hata 200 kwa siku, hawa siwezi kuwafanya waniingizie pesa kwa matangazo, so nikaumiza kichwa na research nikaamua niwe nauza products na maarifa yangu.

nilianza kuandika vitabu vya page 8 hadi 10 navisave kwenye pdf nauza elf 10 naviambatanisha kwenye blog pamoja na namba yangu ya whatsapp naviuza, mwaka huu baada ya requests nyingi za kuulizwa sana ipi original, ipi feki, ipi inafaa, n.k, nimeanza kuwauzia bidhaa kwa order kwa faida nzuri, huwa naziacha sehemu wanazipitia , ningekuwa na muda zaidi ningeanzisha group la whatsapp kwa ada ya uanachama ila shughuli nyingine zimenibana.
 
Blog Yako inahusiana na masuala ya burudani?
Nop, nipo kwengine, cha muhimu ni kudeal na kitu ambacho una maarifa nacho, andika hata post 2 tu kila wikiziwe zimeshiba ila uwe consistent usitoke sana nje.

mfano kama unapenda magari jaza blog yako na post kama

  • Jinsi ya kutunza gari lako ili lidumu kwa muda mrefu
  • Makosa ya kuepuka unapofanya matengenezo ya gari
  • Kununua IST au Vitz, faida na hasara ya kila gari
  • Gharama za matengenezo ya gari Tanzania
  • Jinsi ya kuchagua oil bora kwa gari lako
  • Dalili za matatizo ya injini na jinsi ya kuyatatua
  • Jinsi ya kutunza betri ya gari ili isiharibike haraka
  • Namna ya kuokoa mafuta kwa gari lako
  • Jinsi ya kutambua dalili za clutch mbovu kwenye gari
  • Vidokezo vya matengenezo ya breki kwa usalama wa gari lako

wasomaji automatically wanakuona umebobea, utaanza kuulizwa maswali, kuombwa ushauri, n.k. hapo unaweza kuchapa kitabu chako unakiuza kwa mfumo wa pdf, unaweza kujumua carton za oili unauza rejareja, n.k.
 
Blogging sio kazi yangu, naweza kusema ni kama aina ya mti nilioupanda mimi navuna tu, nina shughuli zingine

Watu wengi wanapofungua blog wazo linalowajia, ngoja nifanye kama blogger flani niposti habari za michezo, miziki, udaku, n.k. hapa ndipo watu wengi sana wanafeli na kuzifunga blogs zao kwasababu zinakosa watembeleaji

Out of nowhere ufungue blog ya ajira ni ngumu kushindana na kina Millard ayo na magwiji wengine, utapigwa kanzu hasa ukizingatia wao wana majina tayari na wamesomea uandish wa habari na wameajiri vijana.

Bloggers wakubwa vipato vyao wanategemea matangazo, mfano blogger maarufu anapata watazamaji laki kila siku, kampuni za hapa hapa kwetu zinaweza kumuomba atangazie biashara zao kwa dau flani lets say milioni kila mwezi, ni kampuni moja tu hilo. unakuja kwa google hawa wanalipa kama dola 1 kwa kila watazamaji elfu moja ambayo ni sawa na shilingi 2,500, so matangazo yanafaa zaidi bloggers wenye watembeleaji

mimi nilianzisha blog yangu kama hobby tu, kuandika vitu ninavyovijua kwa undani, nilikuwa napata viewer kama 10 tu kwa wiki, baada ya research binafsi nikaona nijikite na kitu kimoja tu ambacho tupo bloggers wachache sana, yani blog iwe imejaa taarifa au habari za kitu flani tu mwanzo mwisho,

Kwa mfano blog iwe inazungumzia chunusi tu, unajaza posts kama
  • Vipodozi bora kwa ngozi yenye chunusi
  • Njia za kuondoa chunusi kwa haraka
  • Sababu za chunusi na jinsi ya kuzizuia
  • Vipodozi vya asili vya kutibu chunusi
kama unapenda magari
  • Jinsi ya kutunza gari lako ili lidumu kwa muda mrefu
  • Makosa ya kuepuka unapofanya matengenezo ya gari
  • Kununua IST au Vitz, faida na hasara ya kila gari
  • Gharama za matengenezo ya gari Tanzania
Blogs kubwa kuna muda huwa zinachapisha hizi posti lakini tofauti ni kwamba mimi nimejikita zaidi na kitu kimoja tu na muhimu zaidi kuna blogs chache au hakuna kabisa zinazungumzia chunusi tu, kwenye matokeo ya google mdogo mdogo unaanza kupewa kipaumbele kwenye matokeo ya chunusi, magari, n.k. google wanapenda sana ukiwa una deal na kitu kimoja tu ila ponea yako competition isiwe kubwa sana, mfano ukianzisha blog ya simba au yanga cometition ni kubwa, blogs kibao zimejikita huko, nadhani mnanielewa

Muda unavyozidi kwenda nikawa naona napata watembeleaji hata 200 kwa siku, hawa siwezi kuwafanya waniingizie pesa kwa matangazo, so nikaumiza kichwa na research nikaamua niwe nauza products na maarifa yangu.

nilianza kuandika vitabu vya page 8 hadi 10 navisave kwenye pdf nauza elf 10 naviambatanisha kwenye blog pamoja na namba yangu ya whatsapp naviuza, mwaka huu baada ya requests nyingi za kuulizwa sana ipi original, ipi feki, ipi inafaa, n.k, nimeanza kuwauzia bidhaa kwa order kwa faida nzuri, huwa naziacha sehemu wanazipitia , ningekuwa na muda zaidi ningeanzisha group la whatsapp kwa ada ya uanachama ila shughuli nyingine zimenibana.
207-2020 nilifungua ila sikuwa consistent . Ila ni jambo zuri hongera mkuu
 
Hongera mkuu, hapa nilipo naumiza ndonga, ni kitu gani hasa nijikite nacho .
 
Take your time , fanya utafiti ..

With more info unaweza kufanya maamuzi Bora zaidi kiongozi
 
Niko na makala 200 nishaziandika hadi sasa nikioata free time ni kuandika tu. Nikianza kuzipandisha ni kuzipandisha tu mdogo mdogo huku bila kutolea macho pesa ya haraka.
 
Mpaka uanze kutengeneza hela miaka 10+ mbele ukianza leo focus yako iwe 2035-2040
 
Back
Top Bottom