Standards Person
JF-Expert Member
- Apr 22, 2021
- 672
- 860
Bila kuwachosha wanajukwaa nitaandika kwa kifupi sana. Juzi waziri wa Tamisemi na mbunge wa Tanga alikuepo jimboni kwake. Kupitia mitandao ya kijamii nimeona eti akiwapongeza viongozi Tanga kwasababu hawagombani.
Naomba nimwambie hawagombani kwasababu lao ni moja (kuinyonya Tanga). Unadhani mtu kama Anthony Mtaka au Yule RC Mwanza, Geita, ambae hajulikani kwani hatatui kero za wananchi. Au Takukuru waliolala wakati mji unafwonzwa? Halafu eti mbunge kabisa unasifiatu kutogombana.
Ummy anajua kabisa kwamba mkurugenzi anaingilia michakato ya ujenzi na anatuhumiwa kwa rushwa. Anajua wapo watumishi waliofukuzwa kazi na wake zao wanachukuliwa hapo halmashauri. Anaijua tuhuma ya rushwa ya ngono anajua watumishi waadilifu walivyonyanyasika.
Ndani ya halmashauri kama sio mpigaji unaambiwa kabisa kwa usalama wako hama ukikataa utatengenezewa zengwe ufukuzwe kazi. Ummy anajua bali anajitoa ufahamu. Ninaomba sana kwa Mungu Mh. Rais amuondoe Ummy kwenye uwaziri maana anafanya upendeleo anaondoa wakurugenzi wa halmashauri nyingine halafu kwake kumeoza.
Amewaondoa kazini kwa hoja kwamba wananchi wamelalamika. Atupe utaratibu wa kulalamika kama ni barua tuandike kwa katibu mkuu au popote.
Ummy anajua watu wameporwa viwanja na wengine maboma yao. Watu wameingiza maji na wanalipia lakini kiwanja kinauzwa kuna kesi za ardhi lukuki leo unawachekea chekeatu, kwanini? Ni ubabe wao au aliwatuma? Ummy hana huruma na wananchi wake. Wenye huruma na wananchi akina Sele Bosi hawatakiwi ndani ya halmashauri na wakamfanyia fitna asiingie kwenye umeya.
Ummy anawatetea kwa kua anaona wamemuweka ninamwambia kama Mungu akimtia tamaa ya kuomba tena ubunge hawatakuepo hao hapo ndio ataelewa kama dunia duara. Atawafuata wamsaidie kampeni? Hakuna kiongozi yoyote kutoka tanga atakae mlalamikia mkurugenzi aliepo kwani lao nimoja.
Ummy aondolewe kwenye uwaziri kwa maendeleo ya wanatanga maana anafanya upendeleo.