Pole sana kwa yaliyokusibu smile,mimi ushauri wangu ni kuwa uwe mwangalifu tu,usije jiingiza kichwakichwa kwa jamaa na kama yeye lengo lake ni mzigo tu akishabanjua ndo humuoni tena,kaa na huyo jamaa na jadilini dhamira zenu,kama kweli anakupenda kwa kukuoa hilo ni sawa lakini kama anataka tu mzigo tumia akili ya kuambiwa kisha changanya na zako,cheki na jamaa ujue previous relationship zake,je sasa ana mke au hana?kama ana mke mkimbie kama ukoma unless unataka kuwa mke wa pili au nyumba ndogo,mwanaume ana ushawishi mkubwa mno katika suala la mapenzi na hasa akigundua ulishawahi kutendwa,kwani atajifanya anakujali na wewe utaona mtu ndo huyu lakini ukimpa tu utaona changes vinginevyo awe na dhamira ya kukuoa.
Kitu kingine epuka kumpiga mzizinga kwani hiyo ndo imekuwa tabia ya kina dada,utaona mtu akishakuwa na uhusiano na mtu atataka shida zake zimalizwe na huyo bwana hata kama nayeye ana kazi,hilo huwa ni kosa kubwa kwani kama mtu hana dhamira nawe atakuhonga kiasi ukitakacho hata gari,lakini akishakula tu anza kuhesabu maumivu.
Please take care!