Ninampenda sana Diamond Platnumz kwa sababu......

Ninampenda sana Diamond Platnumz kwa sababu......

queenkami

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2010
Posts
1,694
Reaction score
1,249
Kitu ambacho kinanifanya nimpende Diamond ni jinsi anavyompenda,mjali na kumuheshimu mama yake.
Mimi kama mwanamke natamani siku nikiwa mama mwanangu anithamini kama ambavyo Dimond anamdhamini mama yake.Nilipenda jinsi anavyokwenda kuchukua baraka kwa mama yake kabla ya kwenda kwenye show zake.

Honestly mimi siamini kama Diamond ni mshirikina,kinachompandisha Diamond ni baraka za mama yake.Kama diamond angekua anafanya vitu vya kumsononesha mama yake na yeye angevuma kidogo tu nakuporomoka kama wenzio.

Pia ukweli Diamond ana sauti nzuri na ni mbunifu.
Kitu anachoniudhi Diamond ni vile alivyoonesha ule mboxer mweupe mbali ya hapo tukimsuport anaweza kufika mbali sana ktk ramani ya muziki wa kimataifa.

Kati ya nyimbo zake ninazozipenda ni Nitarejea.Mashairi ya ule wimbo ni mazito ukiyatafakari kwa undani yanatuhusu sana watanzania.
 
Mi pia namkubali sana Diamond, akiwa stejini anajua nini kaenda kufanya!!!!!!!
sio wasanii uchwara kazi kushika suruali kwa mbele maneno yao ni "ooohhyeeeeaaaa piga keleeeee"
nyambaffff tumekuja kupiga kelele au kuona unapafom
 
Me kile kiuno tu ndo chanimaliza.
Huwa najiuliza siku itakuwaje...
Nampenda sana jamani.
 
umeona eeeh Diamond lazima akimbize hao wengine bangi tu maneno meeengi perfomance sifuri.
 
Me kile kiuno tu ndo chanimaliza.
Huwa najiuliza siku itakuwaje...
Nampenda sana jamani.
hahaa madam naona uko hoi bin taaban.
mimi nampendea ''Heshima na Upole
na busara alizoridhi
kutoka kwa mama yake''
 
Kitu ambacho kinanifanya nimpende Diamond ni jinsi anavyompenda,mjali na kumuheshimu mama yake.
Mimi kama mwanamke natamani siku nikiwa mama mwanangu anithamini kama ambavyo Dimond anamdhamini mama yake.Nilipenda jinsi anavyokwenda kuchukua baraka kwa mama yake kabla ya kwenda kwenye show zake.
Honestly mimi siamini kama Diamond ni mshirikina,kinachompandisha Diamond ni baraka za mama yake.Kama diamond angekua anafanya vitu vya kumsononesha mama yake na yeye angevuma kidogo tu nakuporomoka kama wenzio.
Pia ukweli Diamond ana sauti nzuri na ni mbunifu.
Kitu anachoniudhi Diamond ni vile alivyoonesha ule mboxer mweupe mbali ya hapo tukimsuport anaweza kufika mbali sana ktk ramani ya muziki wa kimataifa.
Kati ya nyimbo zake ninazozipenda ni Nitarejea.Mashairi ya ule wimbo ni mazito ukiyatafakari kwa undani yanatuhusu sana watanzania.
hata uche utampa
 
Kuperform anajitahidi hasa lakini pia Mhhh kiatu usichokivaa huwezi kukisemea na hapa namaanisha kuhusu ushirikina...... how sure are you kwamba sio? kijana wa tandale kwa mambo hayo ndio wenyewe.......
 
Huyu kijana kweli ni mzuri na hata ukienda kwa show zake wala hujutii kama hawa wengine, anakuhamasisha kuendelea kumtizama mwanzo wa show hadi mwisho. Nampenda pia.
 
Wadada tena wata acha kumpenda akati ndo sukari ya warembo. Hapa waschana ndo wanasema wana mpenda sana.
Kwerih almasi yupo njema sana yupo safi sana na pia anakimbizaa game na kubadilisha mzik wa tz katka levo sawia.
 
Kuna jibaba flani liliwahi kusema humu JF kuwa linampenda jinsi alivyoonyesha masaburi yake kwenye show ya fiesta.
Dah! Nimeamini huyu jamaa anapendwa sana.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
huyu kijana hana adabu kwa binti za watu

Kila mtu ana madhaifu yake na mazuri yake.
Nampendea mazuri yake niliyoyataja.
Hata hivyo binadamu hawakosi la kusema ndo maana hata mitume wa Mungu Yesu na Muhamad kuna wanaowasema vibaya itakua Diamond.
Nina imani angekua hataki mabinti mngesema ni punga,mi naona bora ajifaidie hao mabnti kuliko angekua punga.
 
nimefurah vile raia wamemuunga mkono mtoa mada
nilitegemea kuponda kma jadi yao

Palipo na riziki\mafanikio hapakosi chuki mkuu.
Kadri Diamond aka jiwe la mwadui atakavyopanda ndivyo msururu wa haters watakavyoongezeka.
Hao wanaoponda hawanishangazi sababu mti wenye matunda ndio utupiwao mawe.
 
Kuperform anajitahidi hasa lakini pia Mhhh kiatu usichokivaa huwezi kukisemea na hapa namaanisha kuhusu ushirikina...... how sure are you kwamba sio? kijana wa tandale kwa mambo hayo ndio wenyewe.......

Mimi nina amini hapandishwi na ulozi sababu kwanza kabisa siamini kama hayo matakataka yanafanya kazi.
Yangekua yanafanya kazi risasi za mjerumani zingeyeyuka kuwa maji enzi za kinjeketile Ngwale.
Pili ili msanii afanikiwe inabidi awe na sauti nzuri,mashairi mazuri ajue kulitawala jukwaa na pia awe mbunifu vitu ambavyo Diamond anavyo na vinaonekana kwa macho na masikio lkn huo uchawi hakuna ushahidi unaoweza kudhibitisha.
Nyimbo kama mbagala na nitarejea hazitakaa zichuje sababu ya ujumbe uliopo ktk mashairi yake.
Kijana amezawadiwa alichonacho na Mungu na hakuna binadamu anayeweza kumshusha si kwa maneno wala kwa kumsingizia kuwa ni mlozi.
 
Back
Top Bottom