Ninani anamshauri Rais kuhusu Hali ya uchumi wetu? Miradi inayoanzishwa inaendana na uhalisia wa uchumi wetu? Wataalam wa uchumi mpo wapi?

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Huko twita mtifuano unaoendelea ni kuhusu tozo...tozo za miamala ya simu ,na tozo katika taasisi za kifedha. Huku mtaani mnyukano uliopo ni kupanda Kwa gharama za maisha,na Hali mbaya ya chakura nchini. Kule Kwa waziri wa fedha kinachoendelea ni majibu ya kibabe kwamba tozo ni sheria na ni msahafu hawezi kubadili katu maana tozo ipo kisheria . Kwenye miradi Nako sgr kipande Cha dar -moro mpaka Leo hakijaanza kazi ,achilia mbali kuanza kazi hata train yenyewe na mabehewa yake haijulikani itawasili lini. Kabla hatuja maliza kipande Cha dar -moro Kuna kipande Cha Moro -dodoma -,. kabla hatujamaliza kipande Cha Moro -dodoma kimeanzishwa kipande Cha dodoma mwanza ...,na kabla ya kumaliza kipande Cha dodoma mwanza kimeanzishwa kipande Cha kisaki - tabora -kigoma zote hizi eti ni SGR . najiuliza nchi hii inawashauri wa kiuchumi au ni waziri wafedha bwana mwigulu ndiye anapuyanga anavyotaka yeye mwenyewe? Bwawa la nyerere halijulikani mpaka Sasa litakamilika lini. Kwanini tusiwe na utaratibu wa kumaliza jambo Moja kabla hatujaanza lingine? Kwanini SGR isiishie dodoma kwanza ikamilike na ianze kazi tuuone ufanisi wake ndipo tuendelee na maeneo mengine? Kwanini mwanza isijengwe kwanza reli ya kawaida na hii ya tazara iboreshwe Kwa kuleta train mpya za kisasa ? Kwanini hamtaki kumaliza Moja kabla ya lingine ? Sasa haya matozo hata mkiweka Kila Mahali hamtakidhi matarajio Kwa sababu mmeutwisha uchumi wetu mzigo mzito kuliko uhalisia wake . Tunao wataalam wa uchumi wengi sana je tunao washauri kabla ya kuanzisha miradi mipya? Mwigulu ni kama anajua Kila kitu , lakini ukweli ni kwamba inaonyesha awamu hii imekaa mbali sana na wanauchumi ,,tunao wabobezi katika uchumi ambao wanaweza kutuvusha . Rais wangu Kila jambo Lina wataalam wake jitahidi kuwa shirikisha wataalam wetu huenda na hizo kelele zitapungua . Tunajua Nia Yako ni njema lakini punda wetu bado ni mdogo msitwishe mzigo mkubwa sanaaa!!! MWIGULU akae pembenj kwanza naona Hana Msaada Kwa taifa zaidi ya kutembea na beji shingoni .tunataka maendeleo yaliyopangiliwa vizuri ,Mimi mganguzi nimemaliza acha nizibe pancha taili ya baiskeli yanguu!!!!
 
Wanakuja kukujibu mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…