Ninaogopa endapo Othman Masoud na Ismail Jussa wataamua kumjibu Tundu Lissu wa CHADEMA kuhusu Katiba ya JMT ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984!

Ninaogopa endapo Othman Masoud na Ismail Jussa wataamua kumjibu Tundu Lissu wa CHADEMA kuhusu Katiba ya JMT ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984!

Kwanini hizo zote hazikuweza kuwashwishi wenye madaraka kuunda Muungano wa Seriali 3

..mabadiliko yanaweza yasi-guarantee Ccm kuendelea kuwa madarakani, au yanaweza kupunguza nguvu yao kwa kiwango kikubwa.

..binafsi naamini kuna mambo Ccm hawataki yaangaliwe, au yashughulikiwe, na mtawala asiyetokana na chamaa chao.

..kwa hiyo huenda Ccm ikang'ang'ania serikali mbili, na katiba ya 1977, kwa muda mrefu mpaka pale pressure itakapokuwa kubwa kupita kiasi.
 
Majibu ya Tundu Antipas Lissu kwa Wakuli Msomi Fatma Karume mjukuu wa muasisi wa Muungano yamenitisha lakini naogopa zaidi kama Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Othman Masoud na msaidizi wake Ismail Jussa wataamua kujibu Mapigo

Kilichonitisha ni kifungu cha Katiba ya Zanzibar kinachosema "Tanzania INATOKANA na muungano wa Nchi mbili"

Tundu Lissu amepigia mstari Neno "inatokana" na akauliza hiyo Nchi ya pili ni ipi?

Tuzidi kumuomba Mungu wa mbinguni aulinde Muungano Wetu!
Huu muungano hauna maana.
 
Huko United Kingdom, Scotland inatamani ijiondoe kwenye Muungano lakini wanakataliwa. Wales na Ireland pia wanajiona wanahitaji kuwa sovereign lakini hawajarusiwa kuwa independent.

USA zile states 51 ziliunganishwa kwa civil wars miaka ya 1700. Kwa nini wasiziache ziwe pekee?

Russia leo inapigana na Ukraine kutetea wananachi wa Ukraine wenye asili ya Russia kwenye majimbo ya Luhansk na Donestk, yote ni kujiimarisha.

Akina Tundu Lissu au Jussa ni wachache kuliko wengi wanaopenda Muungano.

Mfumo aliouweka Nyerere ulikuwa na faida zake na hasara zake. Kikubwa ni kuzipima tu whether hasara ni kubwa kuliko faida
Hatuutaki muungano!!
 
..hapana.

..Samuel Sitta, Samia Suluhu, na Andrew Chenge, waliongoza kazi ya kuandika Katiba pendekezwa.

..Na Rais Kikwete alikabidhiwa Katiba pendekezwa kama hitimisho la kazi ya bunge maalum la katiba.

..sasa tujiulize, Katiba pendekezwa iko wapi? Je, ukawa ndio wameficha katiba pendekezwa?
Ndani ya katiba pendekezwa kuna muungano wa serikali tatu?
 
Huko United Kingdom, Scotland inatamani ijiondoe kwenye Muungano lakini wanakataliwa. Wales na Ireland pia wanajiona wanahitaji kuwa sovereign lakini hawajarusiwa kuwa independent.

USA zile states 51 ziliunganishwa kwa civil wars miaka ya 1700. Kwa nini wasiziache ziwe pekee?

Russia leo inapigana na Ukraine kutetea wananachi wa Ukraine wenye asili ya Russia kwenye majimbo ya Luhansk na Donestk, yote ni kujiimarisha.

Akina Tundu Lissu au Jussa ni wachache kuliko wengi wanaopenda Muungano.

Mfumo aliouweka Nyerere ulikuwa na faida zake na hasara zake. Kikubwa ni kuzipima tu whether hasara ni kubwa kuliko faida
Hao wananchi wengi unaowaongelea hapa wanaopenda huu Muungano umewapata wapi au kwa takwimu gani? Kwa upande wa Tanganyika hakuna mwananchi wa kawaida anayeweza kueleza faida ama binafsi au ya kitaifa inayomnufaisha yeye zaidi ya viongozi na chama cha tawala. Huko zanzibz ndiko usithubutu kuuliza faida kwao hawataki kabisa.

Ccm na serikali waruhusu uamuzi wa kura ya maoni juu kuendelea kwa Muungano huu au muundo wa Muungano halafu ndipo utakuwa na uhalali wa kuwasemea hao wananchi.
 
Ndani ya katiba pendekezwa kuna muungano wa serikali tatu?

..kuna serikali 2.

..ni dhana potofu kusema Ukawa walikwamisha mchakato wa katiba.

..ukawa hawakuwa na wajumbe wa kutosha ktk bunge maalum kuweza kukwamisha mchakato.

..vikao vya bunge maalum viliendelea mpaka zoezi la kuandika katiba pendekezwa lilipokamilika.

..inastaajabisha kwamba Ccm wameachana na katiba pendekezwa ambayo waliiunga mkono.
 
Siasa zetu zina ujinga, uongo, ujuha, upumbavu na mengine yanayofanana na hayo. Tunajenga jamii na taifa la namna gani?
Lazima lifanyike jambo ili tuwe na watu wakweli, waadilifu na wenye weledi kwenye siasa kwa mustakabali mwema wa jamii na taifa kwa ujumla.
Na hii ndiyo kazi ya kipaumbele kwa TISS. Au nao ni kama habari ya yai na kuku.
 
Muungano haufi ila watu waachwe waujadili kwa kina, hayo machache tu aliyoyaibua Lissu yamewaamsha wengi - yaani ni kama kachoma kuni mbichi ndani ya shimo..
Muungano unaolindwa na viongoz wachache wa ccm utakufa tu one day,huu muungano ni fake na haujawah kupata baraka za wananchi kupitia kura ya maoni,ni muungano wa Nyerere na Karume
 
..alishindwa kumshauri Mwenyekiti wa chama chake, na Raisi, kuhusu namna bora ya kutatua kero za muungano.

..pia tangu 2021 amekuwa Mwenyekiti wa chama, Raisi, na Amiri Jeshi Mkuu, na ameshindwa kuyapatia ufumbuzi masuala yanayolalamikiwa.

..kwa kifupi Samia yuko pale kwa maslahi BINAFSI, na si kwa maslahi ya Waznz, Watgk, au muungano.
umejuaje kama alishindwa kumshauri Mwenyekiti? Mtu akishauriwa anaweza kuupokea ushauri au la, kwa hivyo hiyo imebaki kama ni theory tu, na hasa kwamba uamuzi siyo wa mtu mmoja peke yake hata kama alikuwa Waziri.
 
Majibu ya Tundu Antipas Lissu kwa Wakuli Msomi Fatma Karume mjukuu wa muasisi wa Muungano yamenitisha lakini naogopa zaidi kama Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Othman Masoud na msaidizi wake Ismail Jussa wataamua kujibu Mapigo

Kilichonitisha ni kifungu cha Katiba ya Zanzibar kinachosema "Tanzania INATOKANA na muungano wa Nchi mbili"

Tundu Lissu amepigia mstari Neno "inatokana" na akauliza hiyo Nchi ya pili ni ipi?

Tuzidi kumuomba Mungu wa mbinguni aulinde Muungano Wetu!
Jibu sasa wewe hapo
 
..kama matatizo na kero ktk muungano wetu zimeshindwa kutatuliwa kwa muda mrefu sababu itakuwa ni uzembe wa Samia Suluhu Hassan.

..kwa muda mrefu alihudumu ktk ofisi ya Makamu wa Rais kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya muungano.

..baada ya hapo Samia Saluhu amekuwa Makamu na sasa ni Raisi. Haiwezekani ktk nafasi zote hizo ashindwe kutupatia uteuzi wa changamoto za muungano.

..Nadiriki kusema Samia ni MZEMBE.
Yeye mwenyewe hajui anafanya nini na anatakiwa kufanya nini
 
Huo muungano ni wa viongozi wa ccm. Hauna chochote cha maana kwa wananchi wa kawaida

Muungano ulianzishwa kwa ombi la Wamarekani, kwa faida walizozijua wao.

Mzee Henry Kissinger, ambaye alishiriki kuutengeneza huu Muungano, bado yupo hai, wataalam wa Hostoria, kaongeani naye, akawape ABC ya Muungano.

Kwa sasa muundo w Muungano urekebishwe ili uwe na tija kwa pande husika. Hofu waliyokuwa nayo Wamarekani wakati ule, sidhani kama bado ipo.
 
Back
Top Bottom