Ninaomba ajira yoyote halali, nina elimu ya Sekondari

Ninaomba ajira yoyote halali, nina elimu ya Sekondari

kama upo dar es salaam....kama unaweza kupata cheti cha darasa la saba...cheti cha kuzaliwa...kitambulisho cha nida...pamoja na wadhamini wawili...njoo gardaworld tunapatikana mikocheni b...kituo kinaitwa kwa mwinyi...kazi hii ni ya ulinzi mshahala unaanzia 250k
Angalia pm yako boss
 

pitia haka kaandiko kameorothesha baadhi ya fursa maana ajira siku hz hazina uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante mkuu
 
kama upo dar es salaam....kama unaweza kupata cheti cha darasa la saba...cheti cha kuzaliwa...kitambulisho cha nida...pamoja na wadhamini wawili...njoo gardaworld tunapatikana mikocheni b...kituo kinaitwa kwa mwinyi...kazi hii ni ya ulinzi mshahala unaanzia 250k
Ahsante mkuu
 
Habarini za mchana ndugu zangu mi ni kijana wa miaka 24.

Na nilikuwa nina malengo makubwa sana kimaisha ila ndoto zangu zilikuja kufifia baada ya baba yangu mzazi ambae ndio alikuwa kila kitu katika familia yangu kufariki nikiwa form 3.

Kitu ambacho kilikuja kufanya niache shule kutokana na ukosefu wa pesa maana mama yupo tu nyumbani hana kazi yoyote.

Nilijitahidi kufanya vibarua na shughuli ndogo ndogo nikaweza walau kujilipia ada ya ufundi wa simu pamoja na compyuter repair pale dit japo kwa nusu coz but mambo tena yakaniendea vibaya ikanidi nisitishe masomo.

Hivyo bac nimekuja kwa moyo mkunjufu ndugu zangu kuomba ajira yoyote iliyohalali inayoweza kupatika ili niendelee pale nilipoishia ukizigatia mama yangu pia ananitegemea namimi ndio hivi bado sina muelekeo.

Najua humu tupo watu tofauti tofauti hivyo naamini hapa nisehem sahihi nayoweza kupata msaada maana hapa jf sisi ni familia moja.

Ansanteni pia karibuni kwa ushauri na maoni mbali mbali.
Pole sana
 
Mwanangu, yaani hiyo fani ya kuchokoachokoa simu za watu ndio Kila kitu! Komaa nayo ! Ukipata sehemu nzuri yenye mzunguko wa hela una uhakika wa kuramba zaidi ya laki Kila siku
 
Back
Top Bottom