Mama Mwana
JF-Expert Member
- Jun 6, 2023
- 2,435
- 7,784
Hamjambo,
Usiku wa kuamkia leo nimeota nipo kwenye mji mwingine, ni kama "lost city" ambapo hakuna mtu lakini majengo yake ni makasri, kama yale kwenye filamu za katuni, mfano jengo la Disneyland.
Nimeota hayo majengo ni chakavu, na nje kuna sanamu za farasi aliyepandwa na mtu akiwa amenyanyua miguu ya mbele kana kwamba anakwenda mbio. Ni kama kuna anayenikaribisha lakini simwoni, nikajiuliza, hapa ni wapi? Nafanya nini hapa? Kwa nini niko hapa?
Nilipoangalia juu, nikaona mbingu ni kama kioo, na ndani yake kuna buibui mkubwa mfano wa nyumba, akitembea na vitu vya ajabuajabu. Nilihisi kuchanganyikiwa. Hayo yote yalikuwa ndotoni, lakini kiuhalisia nilikuwa naweweseka. Mtu niliyelala naye ndiye aliyeniambia leo usiku nimeota na kuweweseka sana.
Nimejaribu kutafakari maana yake, kwani ndoto zangu zimekuwa zikihusiana na matukio ya kweli. Kuna kitu kinaniambia natakiwa kuelewa maana yake. Je, kuna yeyote anayeweza kunisaidia tafsiri ya ndoto hii?