Ninaombeni ushauri, kila ninachowaza kujikomboa kiuchumi sifiki mbali

Nilimuamini mtu ambaye amekuwa akilima vitunguu muda mrefu sana. Ila nilipigwa wakati wa mavuno nikapewa story nyingi, the rest is history.
Unapenda kilimo ila inaonekana kilimo chako cha WhatsApp..ukiamua kulima weka kambi mbamba tu mampa kila stage umo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hahaha yaani watu wanaona ukiolewa ndo mafanikio yako yanapoanzia hii nchi kiboko kabisa ushauri wa ovyo haijapata kutokea
Wasichokijua ndoa inaeza kua pia anguko lako, watanzania ifike sehemu tuache kusakama watu, midomo domo inachangia % kubwa sana kufanya watu waishie sehem isiyo sahihi [emoji35]
 
Kwa ufuta mpaka hapo ameshachelewa labda kama unampa shamba lililo tayari
 
Pole sana kwa hilo nachokushauri focus kwa kile unachoona kitachokusaidia au km huna mtaji tafuta ka ambayo ni halali yenye mtaji mdogo usione aibu.

Maisha ni yako jitahidi sana kila utakachofanya ujiwekee akiba bila kuitoa jiwekee target baada ya hapo utaona matunda yake.

Mimi mwenyewe nilikua muhanga kila siku kichwa kilikua kinauma lkn nilikaa chini nikajiuliza mbona Mungu amenipa kila kitu hali ya kua kuna baadhi wahajakamilika na wanapambana.Nilipata ujasiri mno full kujinyima nlipokua nakosa mpaka hivi leo nashukuru nilipofikia sikati tamaa japo changamoto hazikosekani.
 
Tafuta kwanza mtaji kisha rudi
tukushauri
biashara ya kufanya.
 
Tafuta Maji ya upako ya Mwamposa,uwe unakunywa na kuogea utoe mikosi kwanza.
Alafu huwa hatuanzi kutafuta mtaji kwanza,tunatafuta wazo la Biashara kwanza ambalo ndiyo litaamua uwe na mtaji kiasi gani.
Usipuuze kujilinda kiroho,tafuta maji ya upako!
 
Kama una chura hata usiteseke Sana
 
When everybody is running but don't know why time is running short.........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…