Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 17,929
- 33,764
Ninaona giza mbeleni kwa upande wa Muungano wetu wa Tanganyika +Zanzibar kimuundo na kiutawala.
Tukumbuke kuwa zile zilikuwa zinaitwa kero za Muungano, sasa hivi ni kama hazipo hii ni kutokana na Rais wa Jamhuri kwa sasa ni Mzanzibar-so hope issue nyingi zinashughulikiwa ipasavyo.Ikitokea tena Rais ametoka upande huu wa Tanganyika yamkini mambo yakabadilika kwa kiasi kikubwa na kurudi kule kule na kuanza tena kusikia kelele za wenzetu Wazanzibari.
Hadi sasa tuna Marais 6,ni wawili (2) tu ndio wametoka Zanzibar,itafikia wakati watataka rotation sawia kwenye kiti cha Urais-yani awamu hii Rais akitoka bara basi awamu ijayo atoke Zanzibar-hapa ndipo kimbembe kitaanza
Ikitokea chama chochote kimempitisha Mgombea Rais wa Jamhuri kutoka Zanzibar,hiyo itakuwa sawa na kucheza kamali ni dhahili pasipo shaka Mgombea wa chama pinzani ambacho kina mgombea ambaye atakuwa anatokea bara kitashinda mapema sana.Maana hakuna uwezekano wowote ule mtu kutokea upande wa Tanzania Zanzibar akawa maarufu kuliko wa huku bara katika siasa, na iwapo Serikali au Mamlaka zitatumia ubabe lazima mambo ya October 29 yatajitokeza tena.
Mwaka 1985,wakati mwinyi anachaguliwa kuongoza Tanzania tukumbuke ni miaka 40 sasa imepita.Wakati ule Nyerere ndio alikuwa kila kitu lakini zama zimebadilika-kwa sasa watu wamebadilika kielimu,kimtazamo,kimaarifa na watu wengi ni wasomi. Kwa mazingira ya sasa utawashawishi vipi watu wamchague Rais kutoka Zanzibar wasio mjua-ni jambo gumu sana.
Hata haya yote yaliyotokea October,29 chanzo ni kimoja tu ni Mama kutokubalika huku bara na kuamua kutumia njia za ku force King-kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni Mzanzibari kulazimisha kuongoza Jamhuri ya Tanzania.Vilevile,tukiendelea na huu utaratibu wa Makamu kutoka Zanzibar na Rais atoke bara na kufariki je kama ilivyo tokea kwa Magufuli??
Kunahitajika mabadiliko makubwa ya kimuundo wa uongozi na Katiba kati ya Tanganyika na Zanziba kwenye Serikali na vyama,vinginevyo ninaona zaidi ya matatizo huko mbeleni haya mambo yasipo patiwa majawabu.Mawazo ya Nyerere na wenzake kuhusu huu Muundo wa Muungano kwa wakati ule walikuwa sahihi ila kwa sasa nyakati zimebadilika kabisa.
Serikali chukueni hatua