Ninapata mashaka makubwa kama FBI wamehusika na upelelezi wa Arusha na Zanzibar

Ninapata mashaka makubwa kama FBI wamehusika na upelelezi wa Arusha na Zanzibar

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
Kuna mambo yanajitokeza kwenye upelelezi wa kesi hizi za mauji Tanzania, na kila mara serikali yetu imekuwa ikituaminisha kuwa inashirikiana na FBI na wapo kwenye eneo la tukio wakisaidiana kufanya uchunguzi.

Siamini kabisa kama FBI wamefanya uchunuzi wowote uwe ule wa Zanzibar baada ya mapdri kupigwa risasi au huu wa ugaidi wa Arusha.

Weledi na jinsi FBI wanavyofanyakazi hauonekani kabisa katika utendaji na majibu haya tunayoyaona.

FBI wangetaka kujua chanzo cha bomu, nani kashashi kwanini Arusha mlengwa alikuwa ni nani, nani katoa fedha kufanikisha kitendo kile, nani katengeneza bomu, lilifikaje. Je hawa machalii waendesha boda boda kweli ndio walirusha bomu na kama ni kweli je walikuwa wanajua wanarusha bomu??

Haingii akilini kumg'ang'ania mwendesha bodaboda darasa la saba na upatiakani na sababu za kurusha bomu kanisa. What is motives???!! Nothing does add up.

Na kama bomu ni sio la kienyeji kweli hawa waendesha bodaboda wanaweza kununua bomu???

Sioni kabisa kama FBI wapo hata Tanzania labda kama tunawafuata pale ubalozini na kuomba ushauri halafu tunafanya yetu.

Tusipofanya utafiti wakina tusoshangae wengi wakatumia upumbavu wetu wa kujichakulia adui halafu wakafanya kweli. Na kwasababu tunapenda mzaha haya mambo yanakuwa kila siku.
 
INANISIKITISHA SANA FBI SIO WAJINGA NAMNA HIYO ,KWELI MIMI NI MHANGA WA CRIME INVESTIGATION NAKIRI fFBI HAWAJASHIRIKISHW KWENYE HILI NAZIONA AKILI ZA FORM 4 NA ZIRO ZA MAPOLISI WETU WALIOFELI ZIKIFNYA KAZI .
THEY NEVER DEEP TO THE SOURSE OGOPA SANA HATA WAZIRI WA NCHI ALISIMAMA NAKUMTAJA HUYU JAMAA HATA KABLA YA UCHUNGUZI SO INANIWIA KUSEMA KUWA ,WANASHUNDWA KUSEMA SIO MHUSIKA SABABU PRICIPALY ''YOUR BOSS IS ALWAZ RIGHT ''' INANIUMA SANA
 
Wakuu Good day;
FBI wanashiriki katika jambo waliloitiwa au kukaribishwa na wenyeji. nao huwa wanatoa ushauri makini na ufanisi maalum juu
ya kazi stahiki, lakini huwa hawa CROSS THE RED LINE ambayo huheshimu uhuru wa wenyeji wao. " Tangu 9/11 fBi ipo kila pembe za dunia japo kwa kiwango fulani" kwa hiyo sii ajabu kupatikana 24/7.

quote_icon.png
By Hiroshima
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013

Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.

Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)

Rai hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen. Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika shambulio hilo.

Baada ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Pia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenya na Uganda ambao tunashirikiana nao katika upelelezi wa shauri hilo.

Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha, 4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao zinaendelea kuimarika.

Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa kukamatwa kwa watu hao.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.
 
Kwani hujui? Si usanii kwa kwenda mbele

bila shaka kwani humo ndani ya kanisa lenyewe kuna madudu mengi , kesi kama hizo zikishughulikiwa na FBI itakuwa ni kutafichuka madudu mengi ambayo yatapelekea kanisa kusambaratika.
Hata zile kesi za kule Marekani kwenyewe za kanisa unafikiri hata polisi huchungulia ??Magazeti yakifichua fichua kidogo mara Kanisa hubakia kutangaza kulipa fidia , kwisha

Hiyo ni mafia kubwa

With 1.5 crimes per citizen, Vatican City has the highest crime rate in the world.
 
Tunaishi kwenye nchi inayokera kupita kiasi kila kitu tunafanya mzaha kwasababu kuna watu wanaamini wao hawahusiki. Ni lini tulitegemea Tanzania mchungaji atachinjwa au Padri ataviziwa akienda kanisani apigwe shaba. Lini tulitegemea eti watu wakiwa na hasira wanachoma makanisa?? Ni lini tulitegemea kuna siku bomu litarushwa kanisani.

Hawa viongozi wakiendelea na mzaha huu uhalifu utakuwa na kwa vile wanauwezo wa kubadili nyekundu kuwa nyeusi, kuna siku itafika kunako wenye maneno ya kubadili hizo rangi hapo ndio tutajua.

Nchi yeyote ikichezea usalama wa raia wake ni hatari sana. Serikali ya mzaha inazaa mauti. Hakuna aliyesalama Tanzania chini ya utawala huu dhaifu. Na udhaifu ni wa raisi na watumishi wake wote.
 
Sidhani kama FBI wamehusishwa kwenye uchunguzi huu
Binafsi naamini ni propaganda na kutafuta kuaminisha watu kuwa ni kweli mtuhumiwa ni huyo aliyetajwa.
Wanadhani kuwa tukielezwa kuwa ni FBI au Interpol ndio waliochunguza basi tutaamini na kusahau tukio zima.
Hivyi ndivyo serikali zenye ufuasi wa illuminati zinavyofanya kazi, zinatengeneza matatizo halafu zinajaribu kujifanya ndio watatuzi wa hayo matatizo.
 
Wakuu Good day;
FBI wanashiriki katika jambo waliloitiwa au kukaribishwa na wenyeji. nao huwa wanatoa ushauri makini na ufanisi maalum juu
ya kazi stahiki, lakini huwa hawa CROSS THE RED LINE ambayo huheshimu uhuru wa wenyeji wao. " Tangu 9/11 fBi ipo kila pembe za dunia japo kwa kiwango fulani" kwa hiyo sii ajabu kupatikana 24/7.

FBI huwa ni wapelelezi wa ndani yaani ndani ya nchi yao, most of their expertise is withi the USA. CIA ndio wanafanya kazi za ujasusi nje ya USA. Ndio wanaweza kuwepo ubalozini kwasababu is their teritory. Hata mwaka 98 sidhani kama waliokuja ni FBI, just speculations.

Na kama wanakuja nje ya nchi mara nyingi lazima tukio hilo lihusishe Raia wa USA.
 
nimekupata mkuu, LENGO LAO NI MOJA..... !
 
Tunaishi kwenye nchi inayokera kupita kiasi kila kitu tunafanya mzaha kwasababu kuna watu wanaamini wao hawahusiki. Ni lini tulitegemea Tanzania mchungaji atachinjwa au Padri ataviziwa akienda kanisani apigwe shaba. Lini tulitegemea eti watu wakiwa na hasira wanachoma makanisa?? Ni lini tulitegemea kuna siku bomu litarushwa kanisani.

Hawa viongozi wakiendelea na mzaha huu uhalifu utakuwa na kwa vile wanauwezo wa kubadili nyekundu kuwa nyeusi, kuna siku itafika kunako wenye maneno ya kubadili hizo rangi hapo ndio tutajua.

Nchi yeyote ikichezea usalama wa raia wake ni hatari sana. Serikali ya mzaha inazaa mauti. Hakuna aliyesalama Tanzania chini ya utawala huu dhaifu. Na udhaifu ni wa raisi na watumishi wake wote.

Mkuu umenena vyema japo ushauri wako hauwezi kufanyiwa kazi 7bu ya udhaifu wa serikali na kova akiona ataufumbia macho kwani yeye atakuwa akipita kuangali wachocheze wa kidini tu.
 
NI KWELI CIA wanahusika na upelelezi wa nje ya marekani kwa upelelezi wa marekani.HAWA WATU NI SIRI NA HAWATAKIWI KABISA KUJULIKANA NA SERIKALI YOYOTE DUNIANI KUWA HAWA NI WAPELELEZI WA CIA KWA SABABU HAYO NDIYO MAENEO YAO YA KAZI.
wapelelezi wa ndani ya marekani ni FBI ambao nao hawatakiwi kujulikana mahala pao pa kazi yaani huko marekani.
NA HAWA WOTE FBI NA CIA wana utaalamu mwingi ila wapo vitengo tofauti na wakati mwingine wanabadilishana taarifa.
KWA HIYO MAREKANI INAPOSAIDIA NCHI FULANI HAIWEZI KUWATUMIA CIA kwa sababu hakuna taifa linalotakiwa kuwajua kuwa hao ni CIA.
NDIO MANA OPTION YAO NI FBI.

KIMSINGI HAPA TANZANIA NI USANII TUPU.
mfano:hivi inakuwaje shambulizi limetokea leo,watuhumiwa hawajajulikana,hawajahojiwa,hakuna ushahidi wowote.
KIONGOZI WA SERIKALI ANATOKEZA NA KUSEMA"hili sio shambulizi la kidini na tusilihusishe na dini"
HII NI HATARI KWA NINI WALOPOKE KWA KUTOA MITAZAMO YAO NA WANAKOSA SUBIRA KUSUBIRI UPELELEZI.
hata PENGO pia alichemka.
MLIJUAJE KUWA SI LA KIDINI??
 
KWA SASA NAONA USANII TUPU.
waendesha boda boda ndio wameshainunua hiyo kesi kwa ujira wa buku,buku mbili ama buku tatu kisa walikuwa wakijitaftia riziki yao.
MIMI NAONA HAPO MTANDAO WA HAO WALIPUAJI HAUPO.
waendesha daladala walikodiwa.
ALIYEWAKODI na WALIYEMPAKIA NI NANI NA YUKO WAPI?MBONA YEYE HAJAKAMATWA NA TAYARI MBEBAJI ASHAFUNGULIWA KESI?kama kakamatwa kwa nini yeye hajafunguliwa mashitaka?
TUNATAKA UPELELEZI UTUAMBIE YAFUATAYO.
1.je kuna mashambulizi mengine?ama mipango zaidi ya kigaidi?
2.nani kawatuma?
3.kwa nini wameshambulia tanzania?
4.kwa nini walichagua kulenga kanisa na waumini na si vinginevyo?
5.kwa nini si shambulio la kidini?mana tayari mlishatoa conclusion hata kabla ya upelelezi.

HATUTAKI MAJIBU RAHISI TENA YALE YA KISIASA NA BORA MKAE KIMYA.
habari za kutoa majibu bila uchunguzi YATAANGAMIZA TAIFA.
NB:watanzania wa leo wanaakili hata kuzidi upeo wa viongozi wengi na MAJIBU RAHISI HAYAWEZI KUAMINIKA HATA KIDOGO.
ushauri:viongozi waache kufanya siasa hata panapotakiwa uchunguzi.
 
FBI huwa ni wapelelezi wa ndani yaani ndani ya nchi yao, most of their expertise is withi the USA. CIA ndio wanafanya kazi za ujasusi nje ya USA. Ndio wanaweza kuwepo ubalozini kwasababu is their teritory. Hata mwaka 98 sidhani kama waliokuja ni FBI, just speculations.

Na kama wanakuja nje ya nchi mara nyingi lazima tukio hilo lihusishe Raia wa USA.

FBI na Scotland Yard wa UK wanaweza kuombwa na nchi nyingine kusaidia upelelezi ingawa anga zao ni katika mambo ya ndani ya nchi zao lakini ujuzi wao unaheshimika sana kwenye matukio ya jinai kiasi kwamba nchi nyingine zenye dhati ya kutaka kujua ukweli hupenda kunufaika nao. Tatizo hapa kwetu, Serikali hivi sasa haiaminiki na nia yake hasa ya kutaka jawabu la kweli katika matukio haya ya kigaidi inatia shaka. Hata katika kupambana na masuala kama ya mauaji ya albino, wauzaji wakuu wa madawa ya kulevya nako kuna mchecheto achilia mbali ya ufisadi!

SWALI KUU: Inakuwaje wanatumia jina la FBI kama karata turufu kutuliza mambo? Je Marekani hawaoni tatizo taasisi yao muhimu kuhusishwa na usanii uchwara? Na kama Marekani wamekubaliana na upuuzi wa aina hii basi lazima wanatengeneza super profit katika nchi hii ambayo wako tayari kumezea mauzauza mengi. Ingekuwa Zimbabwe, habari ingekuwa nyingine kabisa.
 
hamna cha FBI wala nini uenda wanachukua askari (pale state within state msasani, US EMBASSY MSASANI) WAKIWAFANYA MA FBI KUTUADAA SISI WATANZANIA AMBAO TUNAOGOPA KUULIZA MASWALI KWANI ELIMU ILICHELEWA HAPA KWETU KWAIO TUNA WOGA SANA.
 
FBI na Scotland Yard wa UK wanaweza kuombwa na nchi nyingine kusaidia upelelezi ingawa anga zao ni katika mambo ya ndani ya nchi zao lakini ujuzi wao unaheshimika sana kwenye matukio ya jinai kiasi kwamba nchi nyingine zenye dhati ya kutaka kujua ukweli hupenda kunufaika nao. Tatizo hapa kwetu, Serikali hivi sasa haiaminiki na nia yake hasa ya kutaka jawabu la kweli katika matukio haya ya kigaidi inatia shaka. Hata katika kupambana na masuala kama ya mauaji ya albino, wauzaji wakuu wa madawa ya kulevya nako kuna mchecheto achilia mbali ya ufisadi!

SWALI KUU: Inakuwaje wanatumia jina la FBI kama karata turufu kutuliza mambo? Je Marekani hawaoni tatizo taasisi yao muhimu kuhusishwa na usanii uchwara? Na kama Marekani wamekubaliana na upuuzi wa aina hii basi lazima wanatengeneza super profit katika nchi hii ambayo wako tayari kumezea mauzauza mengi. Ingekuwa Zimbabwe, habari ingekuwa nyingine kabisa.

Mkubwa nakupa tano.

Ukifuatili data base na habari za FBI kwenye website yao wametaja nchi ambazo wamehi kwenda kuokoa au kushiriki kwa ajili tu ya wananchi wao. Ni kweli ukiwaambo wanaweza kutoa ushauri, au logistics ila sio haraka kama ilivyotajwa Arushwa na Zanzibar. Tukio la Zanzibar la mtu mmoja kumpiga mtu risasi FBI haji.

Anyway na sio balozi zote wapo Afrika wapo balozi nafikiri tatu au nne mmojawapo ni Kenya, South Afrika nk.
 
FBI hawafanyi mistake na upuuzi kama ule!Marekani inabidi kuwaonya hawa Policcm kutumia jina lao kwa manufaa binafsi!intelijensia yetu ilitakiwa iwe na database yake ambayo ina share na UG,KE,SA kuhusu ugaidi na suspects wake,vikundi ndani nchi,mahusioano ya vikundi vidogo na vikubwa!na watu wao...pia wawe na habari za mbeleni nani ni mlengwa kutokana na wakati au wakati wote na kwa nini!ili wakija FBI sasa ukiwapa file wanatingisha kichwa na kuunganisha dots,wanaanzia hapo hapo kujua kila kitu !sasa sisi hatuna chochote,wale watakuja kufanya kwa manufaa yao zaidi.....wataongeza eneo la kuangaliwa zaidi,na track trends za ndani zaidi kuona ni eneo linalotengeneza future terrorist na wanaondoka zao na report kwa faida yao zaidi!sisi tunabakia kukomaa na deiwaka wa vijiweni waliotumiwa na proffessionals na wameondoka bila kuacha tracks ....they are smart!we are.....siasa imeharibu jeshi letu na intelijensia yoote!aibu!
 
bila shaka kwani humo ndani ya kanisa lenyewe kuna madudu mengi , kesi kama hizo zikishughulikiwa na fbi itakuwa ni kutafichuka madudu mengi ambayo yatapelekea kanisa kusambaratika. With 1.5 crimes per citizen, vatican city has the highest crime rate in the world.
duh! akili nyingine bwana....
 
OPERATION FALSE FLAG ndio kitu kilichotokea , kama hujui maana ya neno hilo ingia google u search utaelewa naongelea nini
 
Back
Top Bottom