Ninapata mashaka makubwa kama FBI wamehusika na upelelezi wa Arusha na Zanzibar

usiwe na mashaka na wala usipatwe na mashaka yoyote kwani hujui kuwa nchi ishauzwa hii wewe ngoja nawe huuzwe pia ndipo macho yakio yatafunguka
 
Umesikia sheha Zanzibar kamwagiwa tindikali leo ili hali ile kesi ya kumuua padri inataka kufutwa kwa kukosekana ushahidi.
 
Nilishawahi kuwauliza jamaa zangu hili swali lakini walipuuza.

Niliuliza, kama ni kweli FBI wanakuja, kwa nini itangazwe?

:Shughuli za kipilelezi huwa ni za siri, kulikuwa na ulazima gani kutangaza watakaofanya upelezi huo?

:Je, haikuwa njia ya kuhamisha lawama ili upelelezi usiporidhisha lawama ziende kwa FBI?

:Sio njia ya kuhalalisha udhaifu wa wapelelezi wetu kwamba kama walishindwa mbona hata FBI wameshindwa?

:Haikuwa njia ya kisiasa ya mkuu wa kaya kuonyesha tu kwamba ameguswa sana na matukio hivyo ameamua kuita FBI?

:Wote tunamjua mkuu wa kaya kwamba hapendi kuudhi watu flani flani hivi, Je, haikuwa njia ya kujivua lawama kwamba watakaokamatwa sio yeye bali ni FBI?

Mwisho wa siku naungana na wewe kuwa na mashaka kama kweli kuna FBI katika upelelezi wa matukio ya Zanzibar na Arusha.
 
labda kama kuna rafiki zao wazungu ndio walikuja hapa but hao FBI hawajaja maana ushahidi unaotolewa ni wa kiccm zaidi
 
siasa tupu amna FBI Aliyefka Tanzania hizi mbinu huwa znatumika kutulza jamii...wakrsto waltulizwa ikiamika kuwa marekan ni wafuas wakuu wa ukristo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…