Ninapata milioni mbili kila mwezi nimeomba mkopo nimenyimwa

Simba Mkali

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
620
Reaction score
239
WADAU miye ni mjasiriamali nina uwezo wa kuingiza milioni 2 na pointi kadhaa kwa mwezi kwenye biashara yangu ya kukodisha gari katika hoteli hapa jijini na kuingiza wastani wa milioni 24 kwa mwaka . Nimejaribu mara kwenda Axim Bank, Finca na Akiba Commercial Bank ili kuomba mkopo wa Milioni 50 nimedunda.
Axim Bank waliniambia hawa-deal na mikopo midogo, bali wana-deal na wafanyabiashara wakubwa na kuwakopeshwa kuanzia milioni 100 na kuendelea. Akiba na Finca wao walisema hawakopeshi mtu mwenye gari moja, wananitaka niongeze gari nyingine ndipo wanikopeshe. Binafsi sina uwezo wa kuongeza gari la pili bila ya kupata mkopo. Nikawaambia wanikopeshe ili nikanunue gari la pili niliingize kwenye biashara wamekataa katakata. NIMEKWAMA. TAFADHALI nani anajua sehemu ninayoweza kukopesheka?
 
Samahani wadau siyo Milioni 2 kwa wiki kama kichwa cha habari kinavyosema ni kwa mwezi. Samahani kwa usumbufu.
 
Labda tuungane.. Mie nina nissan patrol inapaki tu maskan, naitembelea kidogo sana sababu mie sio mtu wa misele na mitoko kivile..
 
Unakodishiaje hotel gari? Tupo hii style na bsness basi tujue maana gari inapark tu home.
May be ukiwa open nami nikukodishie upate huo mkopo
Ni gari ambayo ina uwezo wa kubeba abiria. Kwa hiyo nawarudisha staff wao majumbani tu.
 
Simba mkali ...,
Tafuta mshauri mtaalam wa biashara akuelekeze namna ya kufanya biashara.
Ni kweli una biashara, lakini jee..,
1. Umefungua kampuni kupitia Brela ...?!
2. Jee, una TIN ...?!
3. Jee, una account ya Bank ya biashara yako ...?
4. Biashara yako ni ya muda gani tangu uianze ...?

Ukumbuke Bank hawataki mjasiriamali anayeanza biashara leo ..., wanataka mtu, au kampuni yenye uzoefu wa biashara yake kuanzia miaka 3 na zaidi .., na uwe na kumbukukumbu/records za biashara hiyo ..
Eg, bank statement, vat returns au kumbukumbu nyingine za malipo ya kodi ulizolipa ..., mkataba wa ofisi uliyopanga , kadi ya gari lako, BIMA comprehensive cover ...

Jipange Mzee ....
 
Nashukuru sana. Kwa bahati nzuri haya yote nimeshayafanya ni zaidi ya miaka mitatu sasa. Mtaalamu wa biashara ameshanipa ushauri wa kutunza rekodi na kulipa kodi. Bima na kila kitu kipo powa. Labda kama una nyongeza mkuu.
 
Nyongeza ...,
Una collateral ... ?
Una dhamana isiyohamishika .., eg; Nyumba, Kiwanja chenye hati, Hati ya Uwekezaji ktk soko la hisa .. ?!

Kama umewapa yote haya na wamekataa kukupa mkopo ..., labda hiyo Bank haina hela mkuu ...! [emoji23]
 
Nyumba ninayo ila inatambulika na serikali ya mtaa. kiwanja kingine ninacho pia kinatambulika na serikali ya mtaa. Basi.
 
Nyumba ninayo ila inatambulika na serikali ya mtaa. kiwanja kingine ninacho pia kinatambulika na serikali ya mtaa. Basi.
Ukiwa na nyumba isiyo na makaratasi Bank inayoyatambua , hawatakupa mkopo ... Au labda thamani ya mkopo ni kubwa sana zaidi kushinda thamani ya hilo jumba lako la kifahari ...[emoji1]
 
Ukiwa na nyumba isiyo na makaratasi Bank inayoyatambua , hawatakupa mkopo ... Au labda thamani ya mkopo ni kubwa sana zaidi kushinda thamani ya hilo jumba lako la kifahari ...[emoji1]
Sitaki kusema uongo! Nina nyumba yenye thamani sana. Pande za Mbezi ya Kimara.
 
Uliwapelekea na hiyo nyumba bado wakakataa kukupa mkopo ...?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…