Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,503
- 13,463
Nimeona taarifa ya Tanesco kuwa kumetokea hitilafu ya mfumo katika kituo chake cha uzalishaji umeme kwa njia ya gesi cha Ubungo na kusababisha upungufu ya uzalishaji wa umeme kwa jumla ya megawati 268 kwenye mfumo, hivyo baadhi ya maeneo kwenye mikoa yanakosa umeme nyakati tofauti.
Nimempigia mtu yupo Arusha kaniambia hakuna Umeme, Dodoma hakuna umeme, nikapiga Iringa nikaambiwa hakuna umeme! Dar karibu yote hakuna umeme na upungufu ni Megawa 268 wakati uzalishaji wa umeme nchini ni zaidi ya Megawati 1,700+.
Bado najiuliza ni kweli Megawati 268 ambazo zinazalishwa hapo Ubungo ndizo zinasababisha tukose umeme karibu nchi nzima? Au kuna mengine ila hatuambiwi ukweli?