Ninapenda kufahamu kwa mwaka nchi ya Tanzania inatumia tani ngapi?. Je viwanda vya ndani vinazalisha tani ngapi kwa mwaka?. Je gap sugar kwa mwaka ni tani ngapi?. Kuna mantinki gani gani Mhe. Waziri wa Kilimo kuipa Kampuni binafsi kibali cha kuleta tani 410,000?. Je sukari itakayozalishwa na viwanda vya ndani vitauzwa wapi kama kibali cha tani 410,000 kimetolewa kwa kampuni binafsi?. Tuna sera ya kulinda viwanda vyetu Je kwa utaratibu huo tunalinda viwanda vyetu?. Je sheria aliyopeleka Waziri Bungeni ya kubadilisha sera ya sukari haitafanya viwanda vyetu vya ndani kufa?.