Ninapendwa na mbu

Ninapendwa na mbu

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,659
Wakuu mimi huwa hata kama tumekaa watu kumi mbu huwa wananifuata mimi kwa wingi kushinda wenzangu. Hivi ni kwa nini?
 
Utakuwa umerogwa au majani ya bustani yatakuwa kazini.
 
Utafiti ulifanywa na kuonyesha kuwa mwili wa binadamu huwa na uwezo wa kufukuza mbu. Huwezo huo hutofautiana kati ya mtu na mwingine. Watu wenye kinga ndogo huwa rahisi kwao kushambuliwa na mbu. Kwa hiyo mnaweza kuwa watu sita lkn watakao shambuliwa na mdudu huyo wakawa wawili tu.
 
Kwa hiyo mimi yawezekana niko na kinga ndogo mkuu....
 
Utakuwa mtamu zaidi ya watu wengine!
 
Jasho, harufu yako pia inaweza pia kuwa chanzo. Ngoja waje wengine
 
Mkuu dawa yake ndogo sana. Jipake mkojo wa mbuzi. Unakumbuka kule kijijiNI watu wengine hua wanalala na mbuzi ndani ya nyumba, hasa wasukuma,wabena, wahehe na warangi. Utakuta ukilala kwenye nyumba wanamolala mbuzi huumwi na mbu hata kama huna net. Ile harufu ya mkojo wa mbuzi ni NATURAL REPELLENT YA MBU
 
Mbu wanashambulia zaidi mtu mlevi na Mama mwenye mimba. Hiyo inatokana na damu zao kuwa na virutubisho vinavyosaidia mayai yao kurutubika vizuri, kwa hiyo kiasili huwa wanao uwezo wa kuwatambua watu wa namna hiyo.
 
Back
Top Bottom