Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Miss Natafutwa

Senior Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
190
Reaction score
593
Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.

Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.

First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.

Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu. Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.

Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.

Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.

Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha 3.
Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza). Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini. Pia nahitaji kumalizia nyumba

Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.

1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.

2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu), Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro.

Asanteni.
 
Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.

Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.

First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.
Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu.

Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.
Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.
Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.

Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha 3.
Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza).
Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini.
Pia nahitaji kumalizia nyumba

Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.
1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.

2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu)
Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro.
Asanteni.
nimeumia sana sijui kwa nn
 
Asante sana
Na kinachoniuma zaidi ni kuwa tulizaliwa wawili tu.
Hivyo napambana mdogo wangu amalize shule.
Ndugu yangu ninakuombea mungu ni mwema sana najua unapitia changamoto kali sana ningekuwa na uwezi ningekusaidia mpendwa lakini ndio ivyo ila nina Imani jamiiforum ni uwanja mpana sana nina Imani utapata msaada kupitia jukwaa ili watu watakushika mkono🙏🏽
 
Back
Top Bottom