Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana kipenzi.Pole sana dearest......
Maybe naomba niulize umesema una dip ya education na ulitumia majina ya mtu hapo imekaaje au ndo ile unauziwa jina kuanza form one? Km hukufanya vzr ? Nieleweshe
Asante sana mpendwaPole and All the Best
AsantePole sana mkuu
Asnate sanaPope sana dada, Natumai wenye uhitaji wata kusikia.
Mzee wangu Ushimen, Shimba ya Buyenze, Grahams, Mshana Jr msikilizeni dada yetu hapa
Kama ni 2000 bado una chochote cha kumsaidia ndugu yetu toa neno naye atapona mana matatizo yatampata mtu yeyote awe tajiri au masikiniHapa inabidi sisi vijana wa 2000 tusome comment tu.
Asante sana.Pole sana mpendwa, Mungu akufanyie wepesi kwa kila jambo.
Ungejaribu hata vibiashara vidogo vidogo sokoni.
Rais Samia aliwapa kiinua migongo wafanya kazi feki,wewe hukupewa? Kama ulifanya kazi Kwa miaka SITA namimi ulilipwa zaidi ya 10M ulipeleka wapi?Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.
Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.
First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.
Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu.
Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.
Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.
Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.
Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha 3.
Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza).
Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini.
Pia nahitaji kumalizia nyumba
Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.
1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.
2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu)
Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro.
Asanteni.
Mungu akufungulie milango ya mibaraka 🙏Habari wana Jf kwa ujumla.

Asante sana mpendwa, nashukuru sana.Ndugu yangu ninakuombea mungu ni mwema sana najua unapitia changamoto kali sana ningekuwa na uwezi ningekusaidia mpendwa lakini ndio ivyo ila nina Imani jamiiforum ni uwanja mpana sana nina Imani utapata msaada kupitia jukwaa ili watu watakushika mkono🙏🏽
Huu ni uongo.Asante sana kipenzi.
Hapana, ni kwamba niliuziwa cheti cha mtu aliyemaliza form 4 nikaenda nacho kusomea ualimu ngazi ya certificate na diploma kwa kutumia jina lake.
Kipindi hiko mimi nilikuwa nimemaliza kidato cha nne miaka kama 3 iliyopita na cheti changu kilichomwa moto na msichana wetu wa kazi.
Hivo nilipanda na jina lake mpaka kufikia ngazi ya diploma (katika kujiendeleza) ndipo nikatumbuliwa hukohuko.