Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Pole sana dearest......

Maybe naomba niulize umesema una dip ya education na ulitumia majina ya mtu hapo imekaaje au ndo ile unauziwa jina kuanza form one? Km hukufanya vzr ? Nieleweshe
Asante sana kipenzi.
Hapana, ni kwamba niliuziwa cheti cha mtu aliyemaliza form 4 nikaenda nacho kusomea ualimu ngazi ya certificate na diploma kwa kutumia jina lake.
Kipindi hiko mimi nilikuwa nimemaliza kidato cha nne miaka kama 3 iliyopita na cheti changu kilichomwa moto na msichana wetu wa kazi.
Hivo nilipanda na jina lake mpaka kufikia ngazi ya diploma (katika kujiendeleza) ndipo nikatumbuliwa hukohuko.
 
UDSM walishawahi kutoa Diploma?
Wadogo waje watuambie.

Lakini kwa gap ya miaka yako, huyo si mdogo wako. Huyo ni mwanao. Mtoto aliyepo Form 3 sasa, akiwa mkubwa sana basi ni 18 years.

Hivyo kuna gap ya miaka 24. This is insane.

Kwa nini umeamua kutumia ID ya member maarufu humu jukwaani? Miss Natafuta?
 
Pole sana Miss Natafutwa nashindwa hata namna ya ku kushauri. Lakini zingatia sana kuwa ni mtu wa shukrani kwa kila jambo.

Maisha siku zote hayawezi kwenda vile unavyotarajia. Nakumbuka habari ya Dada wa Mariah Carey alipata mpaka ugonjwa wa ukimwi kwa sababu ya changamoto kama ulizo nazo wewe lengo ni kupambana na haya haya maisha.

Pole sana endelea kuwa na uvumilivu.
 
Rais Samia aliwapa kiinua migongo wafanya kazi feki,wewe hukupewa? Kama ulifanya kazi Kwa miaka SITA namimi ulilipwa zaidi ya 10M ulipeleka wapi?

Si kweli uyasemayo hapa
 
Mungu akufungulie milango ya mibaraka 🙏
 
Asante sana mpendwa, nashukuru sana.
Nina imani wenye uhitaji watanisikia na kunishika mkono.
Nashukuru sana.
Ni changamoto tu za dunia, nina imani zina mwisho.
Asante sana
 
Huu ni uongo.

Kwanza, kinachomata haswa ni index number ya kidato cha nne. Cheti huwa ni nyongeza tu baadae, hapa nazungumzia katika mchakato wa kuomba vyuo, nk.

Lakini pia, ukichoma cheti ama kukipoteza kwa bahati mbaya, utaratibu upo very clear. Omba loss report, andika barua kwenda NECTA, watakutengenezea cheti kingine.

Kudai ulitumia cheti cha mtu kwa sababu chako ulichoma ni upuuzi usio na mantiki.
 
Kwa nini uliacha kujiuza?

Je, ulipata hela za kutosha au ni vipi?

Kwa uamuzi wako wa kuweka kila kitu hapa, ukisema uliwahi kujiuza NA SASA HUTAKI TENA KUJIUZA, umeamua kutafuta kazi.

Huoni kama waajiri wako wanaweza kukusumbua?(Maana past yako inajulikana)

Je huoni kama watu watakutafuta wakiwa na lengo Lao la kificho, wakijaribu kukushawishi kwa hiyo kazi?

Dada, ulikua unajiuza, na kwa bandiko lako hili, muda si mrefu utarudi katika kujiuza hata kama hupendi. Maana hakuna namna, hakuna mwanaume atakutafuta akusaidie kazi tu peke yake behind atakua na interest zake na hiyo ni kwa sababu umewapa past yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…