Nchi ikifikia kuwa na ATM za chakula haiwezi kuwa na maeneo kama hayo.
Piga picha umetoka msalani kama hapo halafu unaingia kupata packaged food bila kunawa mikono, chakula kitashuka kweli?
Si unaweka mlinzi ambaye anakuwa msimamizi wa kituo hicho. Ufungue kituo kariakoo kwa mfano halafu usiweke msimamizi wa eneo si utakuta wamachinga wamepanga biashara zao. Kama unamaanisha vichumba vidogo kama vya benki bado usumbufu utakuwepo kama hakuna usimamizi maana mtu anaweza kuchukua chakula akaanza kula amesimama humo huko, nani atakayemtoa wakati hakuna msimamizi?Hizo gharama nyingine sasa, lengo la ATM ni kupunguza gharama. Aidha, huyo Msimamizi hawezi kuwepo muda wote hadi usiku wa manane.
mpaka hapa ametangaza wameshaiga unafikiri watanzania hawajui hili ni deal poa sana yaani yy mwenyewe ingetakiwa ajipange aandae kisha aanze kuleta hapa kama wazo lililotendeka akileta kama hivi wameshamlia na wameshapata wazo na wanalifanyia kazi
Unawazia watu tu halafu hata mikono wakanawe wapi?
Umetoboa mule mule. That is correct.Siri ya mafanikio ya wahindi waliotoka Uganda walipofika Uingereza ilikua kubadilisha mfumo wa biashara ya chakula. Walianza kufungua migahawa ya 'take away' walichangamikia fursa ya weekend, bank holidays na usiku wa manane.
Nilijaribu mueleza kitu kama hichi unachosema ww that inge work out in drinks & bites tena sehem na sehem i.e. shopping mall, secured public areas....vyuoni etc. Kikubwa hapa bongo miundombinu ndio tatzo.Hizo zipo tayari, zinaitwa fast food (McDonalds, Lotteria e.t.c).. sema wewe unachofanya ni kureplace watu na kuweka machine.
Idea sio mbaya lakini haitofanya kazi, angalia mazingira ya bongo yalivyo, utaweka wapi?
Alafu package hiyo itabidi uikaze kwelikweli maana mtu hawezi amini chakula ambacho katoa tu kwenye machine, ni chakula cha kupika hiki sio chocolate.
Njia pekee ya hii idea kufanya kazi nayoona ni kama utakua na restaurant hii inakua kama extra, au kijibanda ambapo mashine kama hiyo unaweka lakini pia anakuwepo mtu muangalizi wakati wote, kitu ambacho kinatoa ule umuhimu wa machine yenyewe kwa kua kama mtu yupo si bora yeye tu aserve hicho chakula kuliko kusumbuka kutengeneza machine.
Na watu sio tu kununua chakula, wengi ambao wanataka full menu ni wale ambao wanahitaji na sehemu pia ya kukaa kula, sehemu kama mjini hivi umesema kariakoo mtu anunue alafu ale kasimama?
dah sasa mkuu kunishambulia kule, hadi huku kisa ni kitu gani?kwa akili hii ndio maana uko vile