Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Miss_Mariaah

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
2,176
Reaction score
4,979
Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
 
Chukua mwanangu, alafu toa 10M katengeneze Tent za kukodisha 5, kwa mwaka jiwekee kurudisha mkopo kwa kiasi cha 10M ndani ya biashara zako tu. Tent pekee kwenye hio 10 zinakupa 5M, hio 5M nyingine angalia 40M utaiwekeza wapi.
 
Nataka niifanyie uwekezaji
Hapana mkopo unatakiwa uuweke kwenye biashara inayoendelea tayari yaani uongeze liquidity, huduma, bidhaa n.k ila sio kwa uwekezaji mpya. Ni risky sana kufanya kitu kama hicho maana mpaka uwekezaji uanze kukulipa riba inapanda tuu utajikuta 50% ya faida latika miaka hii 9 inaishia kwa riba na hapo ni kama biashara itakua ina exist in 9 years!!
 
Back
Top Bottom