Ninataka kuwa kuwa nyumba container

Ninataka kuwa kuwa nyumba container

0806454469.jpg
 
Gharama ya kununua hilo container mpaka kulidesign liwe nyumba itazidi hiyo mil 2 bado changamoto za joto.Sikushauri.

Kiwanja unacho hiyo mil 2 inatosha kujenga room 1 ya wastani ya kuanzia maisha..
Unainua toka kwenye msingi kozi 8,
kisha kwa sasa usifunge mkanda kwa juu kupunguza gharama ,unalaza mbao na kupiga bati za kawaida ndani utaweka rough floor tu.
Baadae ukipata pesa unatoa bati unafunga mkanda juu,kuezeka na kupaua design unavyotaka.

Kama unafamilia na watoto wadogo chumba jenga kikubwa kiasi kati unaweka zako pazia watoto wanakuwa na sehemu yao.

Ujenzi na finishing ya nyumba ya ndoto yako utakukuta mbele ya safari
 
Bei ya container inachezea milion 4 mpaka 8, badokulitengeneza yani liwe mpaka zile nyumba za wazungu unarudi kule kule kwenye milion 30-40 maana lazima uweke vizuia joto, la sivyo kipindi cha joto ni jehanamu na kipindi cha baridi ni friji
Sasa hapo unampoteza mazima,yeye hafanyi kana kwamba anataka kuonyesha watanzania kuna mpango wa container na nyumba inakua five star, noo anataka kuishi tu ki style kwasababu ya kiuchumi, sasa unataka aweke makorokocho nengii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]halafu container hata 1m unapata
 
Sasa hapo unampoteza mazima,yeye hafanyi kana kwamba anataka kuonyesha watanzania kuna mpango wa container na nyumba inakua five star, noo anataka kuishi tu ki style kwasababu ya kiuchumi, sasa unataka aweke makorokocho nengii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]halafu container hata 1m unapata
Lakini kwa maelezo yake anafikiri container ni chini ya milion 5 wakati ulinunua tu ni kati ya milion 4-8 kutegemea ni futi ngapi. Halafu huwezi kuishi bila kuweka material za kuabsorb joto kipindi cha baridi na kuretain joto kipindi cha baridi.
 
Kontena za chuma(Corten Steel) ambazo ni nyingi sikushauri utumie ingawa zina life span kubwa. Sababu mpaka ikamilike itakugharimu Sana.

Ungetumia kontena za refrigeration, au project yako tafuta tela za Fuso/Canter zilizo kuja kama refrigeration truck/frozen truck hizi ukipata iliyopata ajali utanunua Kwa bei ndogo wewe utafanya mabadiliko kuweka dirisha na mlango.

Kuhusu joto hizi nyingi ni material ya aluminium wewe utaweka cotton insulation kuzuia joto na maisha yataendelea.
 
Mkuu utakuja kujuta nunua tofari kama unaharaka jenga chumba kimoja japo kinaweza kisiishe kwahela hiyo
 
Pale tegeta nikipita nayaona barabarani, kuna watu wanaitwa Ando kama sikosei. Mengine washa design kabisa kama nyumba/ofisi. Ila sijui bei zake.
 
Bei ya container inachezea milion 4 mpaka 8, badokulitengeneza yani liwe kama zile nyumba za wazungu unarudi kule kule kwenye milion 30-40 maana lazima uweke vizuia joto, la sivyo kipindi cha joto ni jehanamu na kipindi cha baridi ni friji
Kwa gharama hizi ajenge tu ya bati chini hadi juu then.
 
Back
Top Bottom