Ninataka nikajaribu hustling Dodoma wakuu

na kipindi cha mavuno

Dodoma wanalima nini?
 
Kule kuikacha Dar tena kwa hoja yenye mashiko,unaonesha unajielewa. Wengi wanaenda huko kwa mkumbo tu.

Juzi tumeona yule jamaa wa Kyerwa aliyefiwa mzazi,kaacha fursa kibao huko kwao kang'ang'ania Dar hata nauli za kurudia kwao tu hamudu na anataka achangiwe kurudi huko!!

Dom fursa nyingi kwa anayejitafuta,asiyechagua mishe.
 
Dsm saa hv ina overpopulation mkuu, imejaa watu wa mikoani, wote kila anayefika anataka afikie kiwandani, afanye biashara kariakoo, kariakoo yenyewe imejaa mpk chalamila kaingilia kati, dar fursa ilikuwa miaka ile kina harmonize wanakwenda kutafuta maisha sio leo, nna dadaang na mumewe wanaishi kwa shida mno huko
 
Naana watu wengi wanaochangia huu uzi hawaijui dodoma, niko hapa dodoma miaka zaidi ya saba, kama unataka kujitafuta sikushauri kabisa, tafuta miii inayochipukia uende huko, Tunduma, kahama, katoro, masasi, na kwengineko, hakuna msimu wa mavuno hapa, hakuna viwanda wala nn, just a salary city, gharama ya maisha iko juu sana hapa, hakuna bodaboda ya buku hapa
 
Kabla hujaja Dom jiulize kwanza ni kitu gani umetafuta / umefanya uko mikoa mingine umekosa na unaamini utakipata Dodoma .

Usije tu eti unakuja kutafuta maisha. Jua kabisa unakuja kufanya nini , unaanzia wapi, una resources gani.

Ukija njoo na life plan Kama hujui unakuja kufanya nini au unafata fursa ipi usije mkuu.

lengo kuu ni kusettle na kutafuta solution ya kudumu. Unaweza ukajikuta 40s inakukutia Domna bado hujapiga hatua. Utahamia mkoa meingine tena.

Life lina gharama sana apo central zone.unaweza ukaishia kupata hela ya kula tu.
 
Ila mzee dsm umeikataa tu ila ni jiji ambalo linathamini juhudi zako ukiwa na akili.

Jiji lisilomtupa mpachapakazi, gharama za maisha ni utake wewe tu ziwe vipi sio kama huko dom kila mtu anakwambia maisha yako juu.
 
elewa kwamba
dodoma inabamba sana kipindi cha bunge na kipindi cha mavuno

dodoma ina mchanganyiko mkubwa wa watu hivyo matukio ya uhalifu yapo sn
Sio kweli. Dodoma ya kuchangamka wakati wa bunge na mavuno ni ileee ya zamani. Sasa hivi uchangamfu ni all season

Matukio ya uhalifu sio makubwa sn.

Natoa ushuhuda huu nikiwa ninaishi Majengo, Dodoma.
 
ila kwa kujitafuta kimaisha sio lazima afikie mjini yapo maeneo kama Kibaigwa, Mpwapwa, Mvumi, Mtumba akipata mwenyeji huko anaweza kuanzia kukaa kwanza pembeni ya mji
Maeneo uliyotaja sio pembeni ya mji Boss. Dom - Mpwapwa ni 105 km. Dom - Kibaigwa ni 101 km. Mvumi nako ni mbali.

Maeneo ya jirani na jiji ni kama Nkuhungu, Nala, Michese, Mkonge, Kikuyu nk. Huko unaweza kupata chumba kwa kuanzia 40k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…