Ninataka nikajaribu hustling Dodoma wakuu

Karibu Dodoma
Njoo uishi Veyula. Kuna vyumba vya 60,000 kwa mwezi. Ni check inbox
 
NAOKUAMBIA USIENDE DODOMA WANA MAMBO HAYA:

Kuna makundi matatu tu ya watu wanaokataa uje Dodoma:

1. Wamefanikiwa wakiwa Dodoma.
Hawataki competition. Wamejenga biashara zao, wamepata kazi nzuri, hivyo hawataki mtu mwingine aje achukue nafasi. Watakuambia "kule hakuna kitu" kumbe wanailinda keki yao.

2. Waliishi Dodoma wakajivuruga wenyewe.
Maisha yaliwashinda sio kwa sababu ya Dodoma, bali kwa sababu ya maamuzi yao. Walitumia vibaya hela, hawakuwa na nidhamu, mwisho wakarudi kwa wazazi. Sasa wanasingizia mji.

3. Hawajafika huko
Wanasikia kwa watu. Anasema kule kuna joto hajawahi kufika hata Bahi. Anasema kule ni mbali kumbe hata ramani ya Tanzania hajui.

UKWELI KUHUSU ISSUE YA MAISHA MAGUMU DODOMA

Watu wengi wanapofika hapa ndipo wanakosea. Wanakimbilia nyumba za bei rahisi bila kuuliza mtaa gani.

Ukifuata huu ndio ukweli:

1. Kila mji una mitaa miwili.
Kuna mtaa wa kawaida na mtaa wa kishua. Dodoma sio tofauti. Ukienda Ilazo, Area D, Medeli utakuta bei tofauti na ukienda Ntyuka au Swaswa.

2. Nyumba nyingi ni mpya.
Tofauti na miji mingi ambapo nyumba ni za zamani, Dodoma nyumba nyingi zina tiles, hazina fangasi, ni mpya. Ndio maana zinaonekana kama ghali, lakini unalipia ubora.

3. Chakula cha 1,500 kipo na ni kingi.
Mipango, Mnada Mpya, Machinnga Complex, CBE, Area 77... vyakula vya 1,500 - 2,500 vipo kila kona. Hata ukienda Restaurant kama Chief Asili bei bado ni nafuu sana ukilinganisha na restaurant kama hizo Arusha au Dar.

4. Usafiri ni rahisi.
Miji mingi usafiri ni bajaji. Hamna boda buku. Dar ndio unaona boda nyingi kwa sababu ndio lango la mafuta.

Dodoma kuna fursa nyingi kuliko unavyofikiria:
Ofisi za Serikali, Vyuo vikuu, Kilimo & Ufugaji, Biashara ya Usafirishaji, na Biashara ya Chakula.

U SHAURI WANGU BINAFSI:

Watu waliokuambia Dodoma chakula ni bei? Wewe nenda kafungue biashara ya chakula.

Waliokuambia usafiri ni bei? Wewe nenda kafungue biashara ya usafiri.

Usisikilize maneno. Nenda kaone fursa.
 
Duh mji wa watumishi huo, ahsante kwa kunisanua mkuu umekaa mbali na unafiki
 
Ila mzee dsm umeikataa tu ila ni jiji ambalo linathamini juhudi zako ukiwa na akili.

Jiji lisilomtupa mpachapakazi, gharama za maisha ni utake wewe tu ziwe vipi sio kama huko dom kila mtu anakwambia maisha yako juu.
Mkuu ni kweli ila kila mtu wa mkoani anakimbilia dar imagine utafutaji unakuwaje japo kila mtu na bahat yake
 
Best comment
 
Ni pazuri utatoboa hadi wanawake za watu maana huko wako single na hawana watu wakuwapa.furaha ni wapweke unakula na mishahara zao na wanavyeoo .
Ukiwabahatisha wawili umetoboa sana wanakufungulia biashara na ist unakula ila uwe mbunifu
 
Fursa za mbeya mkuu ingekuwa vizuri ungezitaja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…