Ninatamani kula wakati wote na huwa napata njaa masaa machache tu baada ya kula, nina tatizo gani?

Ninatamani kula wakati wote na huwa napata njaa masaa machache tu baada ya kula, nina tatizo gani?

Paa

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Posts
1,462
Reaction score
2,935
Mf, nikishakula ugali(Wakushiba kabisa) mchana saa saba mida ya saa kumi kasoro jioni nakua nimeshapata njaa tena.

Nikinywa chai asubuhi saa mbili, saa tano nakua nimeshapata njaa tena.

Pia huwa ninatamani kula kula muda wote

Hii ni shida gani madokta? Na vipi tiba yake?
Maana hali hii sio rafiki kabisa
 
Kwanza Kabisa tafuta dawa ya minyoo kama utadhani hiyo ni miyeyusho basi kapige Faru John ya kutosha then baada ya hapo endelea na mambo mengine.
N. B : Kuna watu wengi sana hawana kabisa appetite sasa wewe mwenzangu umekuja kuanzisha thread
 
  • Thanks
Reactions: Paa

Faru joni ni nini?
 
Dawa ya minyoo uleshatumia?? Maana nimeandika tafuta Dawa ya minyoo ukishindwa kapige FARU JOHN
 
Kapime minyoo na sukari.
Uwe busy na kazi, na kunywa maji ya kutosha ukianza kuhisi njaa.
Yawezekana isewe ni tatizo, ila ni hali ya kupita tu kwa mfano, kuna watu wakiwa na msongo wa mawazo wanakula sana, au wakiwa na hela ambayo hawajaitolea jasho huwa wanawaza sana kula.
 
Back
Top Bottom