Ninatamani kula wakati wote na huwa napata njaa masaa machache tu baada ya kula, nina tatizo gani?

Ninatamani kula wakati wote na huwa napata njaa masaa machache tu baada ya kula, nina tatizo gani?

Kapime sukari yako haraka sana. Ukikuta salama, wahi kwa mchungaji wa Kipentecoste - Sio mtume/nabii akakuombee
 
Mimi Niko tofauti na wew kidogo ! Aisee nikipiga Soda aisee naweza nikahisi Njaa Siku nzima maana ntakuwa nakula baada ya Muda kidogo Njaaa
 
Dawa ya minyoo uleshatumia?? Maana nimeandika tafuta Dawa ya minyoo ukishindwa kapige FARU JOHN
Sijapima nikakutwa na minyoo, sasa naanzaje kula dawa tena
 
Kapime minyoo na sukari.
Uwe busy na kazi, na kunywa maji ya kutosha ukianza kuhisi njaa.
Yawezekana isewe ni tatizo, ila ni hali ya kupita tu kwa mfano, kuna watu wakiwa na msongo wa mawazo wanakula sana, au wakiwa na hela ambayo hawajaitolea jasho huwa wanawaza sana kula.
Sawa bro, nitapima

Ila msongo wa mawazo sina

Na hela ngumu tu kama kawa
 
Back
Top Bottom