Ninatangaza msiba,mama amenitoka

Ninatangaza msiba,mama amenitoka

Pole sana kwa kufiwa na mama mlengwa,umekuja kishairi nikadhani ni andanenga! Umenikumbusha kiswazi mambo ya Edwin semzaba!!
 
Msiba wa mama naujua
Nami nilipita hiyo hatua
Hakika roho huugua
Kama njiwa aliyekosa pa kutua

Mungu amemchukua
Katika wengi kamchagua
Ni kweli kwenu kapungua
Lakini mola ndiye Murua.

Pole sana kaka yangu, Mungu ampumzishe Marehemu mama katika pahala pa salama.
 
pole!!ila ulivyo ileta!!!!mmmmh hivi unapata hata nguvu za kukaa na kuandika wakati mama amekutoka!!
 
Mwenzangu Yakuonea,
Huruma nakuonea,
Janga lilokufikia,
Mungu ndio anajua.

Kwa Mungu nakuombea,
Upate kuvumilia,
Mungu ndo alopangia,
Subira takupatia.

Alazwe mahala pema,
Kwa Mungu afike mama,
Kitapofika kiama,
Tuungane naye mama.

Yote alokuusia,
Usiache timizia,
Wosia kuuenzia,
Heshima tampatia.

Amina tena amina,
Amina tena na tena,
Nasema tena amina,
Tena amina amina.

Mungu alitoa, sasa ametwaa. Mapenzi yake yatimizwe.

RIP our dear mama.
 
Last edited by a moderator:
katika mitihani inayoweza kumkumba mwanadamu mmoja wapo ni pindi akikabiliwa na kifo, na hili ndio lilionikuta mimi,kusema nimefikwa na msiba sidhani kama eti ninataka sifa kama unavyosema au nastahili ban
mi nilidhani ni SHAIRI sbb iko JUKWAA LA LUGHA kumbe ni kweli!..... Pole sana kwa msiba mzito Mwenyez Mungu ailaze roho ya Mama yetu mahali pema peponi
 
pole!!ila ulivyo ileta!!!!mmmmh hivi unapata hata nguvu za kukaa na kuandika wakati mama amekutoka!!

Mkuu ungekua unajua hisia na nguvu ya ushairi, ungejua fika kuwa Yakuonea akikuwa anaandika akiwa na hisia kali (yawezekana chozi likimtoka).

Kila mtu ana njia zake za kumuenzi aliyempenda.
 
Last edited by a moderator:
mi nilidhani ni SHAIRI sbb iko JUKWAA LA LUGHA kumbe ni kweli!..... Pole sana kwa msiba mzito Mwenyez Mungu ailaze roho ya Mama yetu mahali pema peponi

Ni kweli kabisa hilo nilioandika ni shairi na liko kwenye jukwaa la lugha,na hicho nilichokiandika ndicho kilichotokea, sababu hata kama mtu anatumia lugha ya ushairi sidhani kama anaweza kupitiliza mipaka kiasi hicho na kumzushia mama yake umauti
 
Pokea Pole;

Muumba namtajia, jinale nikianzia
Ni kwake tumetokea, na kwake tutarejea

Punguza kaka kulia, machozi pia futia

Ni kwake tutarejea, ni kwake tumetokea


Habari nimepatia, wakati naperuzia

"Bize bize" mimekua, kijiwe sijapitia

Ni leo nimeonea, ni mama kakuagia

Ni kwake tutarejea, ni kwake tumetokea


Mitihani ya Dunia, "mamenu" kuondokea

Za kwake zilifikia, sikuze hapa Dunia
Ni huko twaelekea, Dunia tunapitia
Ni kwake tutarejea, ni kwake tumetokea


Kwa dua namuombea, peponi aje fikia

Matendo yenu murua, nasema yasaidia

Mtani pole pokea, na ndugu pia jamaa

Ni kwake tutarejea, ni kwake tumetokea


Machungu nayahisia, yakwenu kuwafikia

Tupewacho twapokea, hewala twaitikia

Hakuna tunalojua, Muumba twasubiria

Ni kwake tutarejea, ni kwake tumetokea


Wapole mkono natoa, najuu nanyooshea

Mzidi kuaminia, na dua nawaombea

Dunia tunapitia, na hilo nakumbushia

Ni kwake tutarejea, ni kwake tumetokea


Ni mwisho namalizia, Choveki nawaagia

Simanzi inenijaa, fikira zanizidia

Mikono yatetemea, wakati naandikia

Ni kwake tutarejea, ni kwake tumetokea


 
Deno AROBAINATISA,maswali najiuliza, Mbona kama una visa,kwa mwenzio nauliza? Au kunao mkasa,nimeliingia giza? Hakika mi sielewi,hebu nifumbue macho!
kiza hujaingia,ila naona kwa masiala vile unaigiza. Huna uchungu wa mwana aujuae zaidi ya mother. Vile msiba wautangaza nikadhani mwenzangu na malimba wapiga. Yangu samahani nitoe nsije nkachomwa mwiba.
 
NI MAMA MILELE.


ni mama atakumbukwa, siku zote duniani
mikoa yote hadi rukwa,mama ndio tumaini
ni wengi walofikwa,yakuonea pata imani
mama ndio nuru,duniani na mbinguni.
 
Pole sana Mkubwa!


Na mama yetu
mwenyenzi
Ampe pumzik
o la milele kati
ka shamba lak
e

Aaameen!
 
Back
Top Bottom