Ninatarajia kupokea milioni moja na laki mbili. Nataka nilime

Ninatarajia kupokea milioni moja na laki mbili. Nataka nilime

miminimama

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2018
Posts
696
Reaction score
1,818
Wakuu zangu,

Mimi ninaishi Kisarawe Pwani nimejiajiri kwa sasa lakini pia nimeajiri vijana wenzangu 8. Sasa ukitoa mambo mengine kuna sehemu nachimbia 10, 000 kila siku kwa madhumuni ya kuwa mpaka December mwishoni nipate kiasi kisichopungua 1,200,000.

Nimeanza kuweka kuanzia mwezi wa 9 mwaka huu na ninatamani sana kulima zao la muda mfupi kama miezi 3 au 4 lakini litakalonizalishia hela nzuri; yaani hiyo million izae walau hata mara 3 au 2.

Ni mara ya kwanza kulima nahitaji ushauri wenu kwa kuzingatia majira ya mwezi wa kwanza, aina ya zao mpaka navuna kupeleka sokoni.

N.B: Nitakuwa na balance ya kuongezea kidogo ikafika mpaka 1,500,000.

Ahsanteni sana.
 
Ngoja na mimi nisikilize hizo shauri.
 
Kila la heri. Lakini ukienda na mawazo hayo. Sidhani kama utafaulu. Kilimo kinahitaji utulivu sana hakuna faida ya haraka hivyo. Yaani mara 2 hadi 3 ya mtaji?
 
Ndo maana nikaleta kujadili lakini kuweka million kwa muda wa miezi 3 mpaka 4 ikaleta hiyo pesa ni very reasonable.
Kila la heri. Lakini ukienda na mawazo hayo. Sidhani kama utafaulu. Kilimo kinahitaji utulivu sana hakuna faida ya haraka hivyo. Yaani mara 2 hadi 3 ya mtaji?
 
Kila la heri. Lakini ukienda na mawazo hayo. Sidhani kama utafaulu. Kilimo kinahitaji utulivu sana hakuna faida ya haraka hivyo. Yaani mara 2 hadi 3 ya mtaji?
Kuna sehem inawezekana kabisa tatizo ni muda na aina ya zao atalopanda tu.
 
Kilimo mpk upate hasara misimu mitatu/minne ndo utoboe.

Ndio maana kinaitwa uti wa mgongo.
Kuna mrejesho huo si mbaya ukapitia mimi nataka kujua zao la kupanda kwa miezi hiyo mpaka mwezi March au april niwe nishavuna
 
Kwa huo nsimu wa January mpaka March au April mazao hayo yanafaa mkuu? Ngoja nisome utafiti kidogo juu ya ushauri wako nitakurejea.
Nashauri ulime ekari 2 ya pilipili hoho

Au lima nyanya ekari 1.5

Au lima mahindi ya kuchoma ekari 2

Hiyo hela inatosha kabisa na inabaki ya kukulinda
 
Sawa mkuu,all the best.
Kuna mrejesho huo si mbaya ukapitia mimi nataka kujua zao la kupanda kwa miezi hiyo mpaka mwezi March au april niwe nishavuna
 
kilimo kina mambo yake kwahiyo ni vema ukafanya uchunguzi wa eneo unalotaka kufanya kilimo, hasa kujua ni zao gani linashamiri eneo hilo. baada ya zoezi hilo angalia soko la zao hilo limekaaje.

mambo ya kuzingatia, ukishajua zao utalolima basi fanya ujue gharama zake kwa ekari 1 kuanzia ulimaji, kama mbolea, utoaji magugu au maotea, ikiwezekana hadi uvunaji na usafiri upoje.
ni vema ukawa na malengo ya muda mfupi na mrefu ili kujiepusha na "kilimo nyemerezi"
 
Back
Top Bottom