Okay safi sana kilimo ni hela sana...mimi nakushauri usilime mazao ambayo kila mtu analima, yani mazao ya mkumbo. Maana kuna watu wakisikia matikiti yana hela wote huko, mara mahindi yana hela nao wote huko jambo ambalo mwisho mnalima wengi na soko ndio hivyo hela ndogo.
Nakushauri kwanini usilime zao kama soya, soya ni muhimu sana kiafya na ni zao ambalo linavumilia hali zozote. Soya hustahimili ukame, udongo wa tifu tifu pia unalima hadi udongo wa mfinyanzi. Matunzo yake ya kawaida sana, magonjwa makuu ya soya ni ukungu na bacteria tu. Ambazo kuthibiti bacteria kutumia kilimo cha mzunguko yani crop rotation. Haya mbolea hahitajiki sana katika soya ni inategemeama na rutuba ya udongo unaolima. Fanya utafiti kuhusu soya, mazao ambayo hayazingatiwi sana na watu soko lao linakuwaga zuri sana sana. Ama kwa hakika ukifuata huu ushauri na ukaacha kulima kwa mkumbo kama wengine, utaona kilimo ni bora sana