Ninatoka jasho sana, nifanyeje?

Ninatoka jasho sana, nifanyeje?

Amarosa

Member
Joined
Jan 13, 2018
Posts
32
Reaction score
23
Wasalaam, kutokwa na jasho ni kitendo cha kiafya ila ikizidi inageuka kero na kukosesha amani.

Huwa najisikia ovyo sana kuona nguo yangu imeloa jasho sehemu ya kwapani kwa jua la sasa yani nguo hadi mgongoni inaloana, bad enough nakua naenda kazini yani sipendi hii hali nakuwa sina amani kuloana hivo tena kazini.

Msaada wenu please
 
Tumia antiperspirant naskia ndio zinazuia jasho kutoka
 
Pole mkuu,nakuvutia picha unavyoandika huu uzi huku umeloana kwapani hapo
Tumia antiperspirant if ni too serious nenda kwa wataalamu,
 
Pole sana mkuu kwa hilo jasho. Hamia mbeya au jombe utapona
 
Angalia mafuta au lotion unayotumia huenda ndo chanzo kikubwa...kuna ambayo inafanya ngozi iwe dry na kuna inayofanya iwe wet badili hivyo accordingly!!
 
Hiyo ni nature ya ngozi yako.

Muone mtaalamu wa ngozi akupe ushauri mzuri zaidi.

Mwenyewe nna ngozi kama yako, nimeamua kuachana na kabisa na mambo ya lotion na mafuta ya aina yeyote.
 
Angalia mafuta au lotion unayotumia huenda ndo chanzo kikubwa...kuna ambayo inafanya ngozi iwe dry na kuna inayofanya iwe wet badili hivyo accordingly!!

Yan mwilini sipaki mafuta, napaka mikono na miguu tu basi
 
Hiyo ni nature ya ngozi yako.

Muone mtaalamu wa ngozi akupe ushauri mzuri zaidi.

Mwenyewe nna ngozi kama yako, nimeamua kuachana na kabisa na mambo ya lotion na mafuta ya aina yeyote.
Sipaki mafuta mwilini nikiwa natoka na hata nikipaka natumia ya nazi
 
Mwenyewe nasweat khaa hadi make up inashindikana ntahama nchi
 
Inawezekana una tatizo linalojulikana kama hyper hidrosis
Tafuta dawa fulani ziara zinaitwa
Oxybutynin hydrochloride 5 mg
Ni vidonge Pharmacy zote
kubwa wanazo
Bei kwa kidonge ni kati ya 800 hadi 1000 tumia 1 kila siku walao kwa mwezi mmoja
 
Kuna mambo kadhaa ya kuepuka .
1. Mafuta unayotumia.
2. Angalia kama una ugonjwa wowote unaokufanya ukooe
3. Utumiaji wa pombe kupita kiasi .
4 .uvutaji wa sigara .
Tiba:
SHABU : haya nia aina ya magadi yanayouzwa kwenye maduka ya dawa za asili.,unaloweka kwenye maji na kunawa maeneo yote yanayowai sana kutoka jasho..
Nimewai kuwa natatizo hilo ila nilijichunguza ilitokana na ulevi wa pombe ...sasa naendelea vyema baada ya kupunguza kidogo
 
Wasalaam, kutokwa na jasho ni kitendo cha kiafya ila ikizidi inageuka kero na kukosesha amani.

Msaada wenu please
Pole sana. Sasa hakikisha kila siku unatafuna (angalau) nusu nazi. Meza lile tui alafu yale machicha tema. Fanya hivi, baada ya wiki utashangaa unamaliza siku nne bila kuoga na hutosikia harufu ya jasho...
 
Back
Top Bottom