Ninaumia moyo kila ninaposikia serikali ya Tanzania imeagiza ndege mpya ya biashara

Na hizo Sherehe za kupokea Ndege Airport pia huwa kuna kipigo cha hali ya chini.
Omba Mungu akusaidie upate nafasi ya kuzipiga Kodi zetu,kuumia au kulaumu ni matumizi mabaya ya akili yako. Jukumu lako ni kulipa Kodi matumizi yake sio jukumu lako
 
Acheni ndege zikuje, Simba na Yanga zitapewa bure kwenda Cairo na Jozi kuwakilisha Taifa.
 
wangekarabati na viwanja vya ndege,kununua ndege bila ukarabati ni sawa na kununua mkoti wakati shati limechanika
 
Hatuagizi mkuu hiyo ni danganya toto, yule kiongozi wa "MALAIKA" ndo aliweka order, hivo lazima tuichulue baba, sasa kwasababu tulizonazo zinatushinda na tunaziendesha kwa hasara.... kwanini hii tusimpelekee huko?!!!!
 
Kweli kabisa....🙆🙆🙆🙆
 
Halafu ndege yenyewe Boeing 737-9 Max hata bure sipandi.
 
Ni afadhali wanunue maboeing hayo kuliko wakigawana pesa hizo kama posho za wao kuhudhuria makongamano, semina, vikao na warsha zisizojulikana
 
Hiyo mikataba alishasaini yule mbwa aliyekufa na akala cha juu,tuko katika utekelezaji tu, SSH wala asilaumiwe
Aliyeandika post hii yuko kama vile ni mtoto mbweha ndiyo maana anaonyesha chuki dhidi ya mbwa.
 
Mkuu Mimi naona serikali wako sahihi,

Kwasababu nyanja ya kiuchumi ndio inayoibeba/inayoiwezesha nyanja ya kijamii.

Ukiangalia katika muktadha wa kipaumbele kati ya kuwezesha/uwekezaji kati ya nyanja ya kijamii(elimu, afya, maji,nk) na nyanja ya kiuchumi(uwekezaji sekta ya usafirishaji, kilimo, madini, viwanda biashara nk.) utakua umefanya jambo la maana sana kama nguvu kubwa utaiwekeza kwenye nyanja ya uchumi kwani faida/matunda yatakayopatikana ndio yatasaidia kuimarisha na kuendeleza mambo/miradi ya kijamii.

Hata hivyo selikali inafanya mambo yote kwa pamoja kila nyanja imepewa nafasi kulingana na umuhimu/uhitaji/kipaumbele.
 
Hukumsikia Bashungwa akitoa taarifa ya ukarabati wa viwanja vya ndege? Vyote viumefikia asilimia 80. Musoma,Dodoma, Mwanza. Baada ya hapo mtapanda ndege hadi mchoke.

Nchi hii usiwaamini wewe sikiliza kisha tambaa zako.
 
Mbona huumii serikali inapojenga barabara, tena barabara za ndanindani huko,

Au kwa sababu unajua kuna mtanzania atakutumia, hata kama serikali haitopata faida, ila kuna mtanzania atanufaika either kwa kupita au kupitisha gari yake, au kupitisha mazao yake.

Ili usiumie kwenye suala la ndege then Fanya assumption ya Aina hiyo, hata kama wewe hautopanda, ila kuna mtanzania ataipanda au atasafirsha bidhaa yake, au ataajiriwa kuihudunia hiyo ndege.

So, hizi zote ni namna ya serikali kusogeza huduma kwa jamii, ni the same na kujenga barabara au hospitali, lazima kuna mtu ataajiriwa kuihudunia na lazima kuna mtu itamfaa,

Ukiweza hivo then hutaumia.

Ila ukiwa na roho ya ubinafsi utaumia kila siku, ukisikia wamejenga daraja la busisi utaumia, ukisikia wamejenga barabara ya songea utaumia, ukisikia wamejenga uwanja wa mpira utaumia..... The list go on and on as long as haikugusi wewe itaendelea kuumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…