Ninaumia moyo kila ninaposikia serikali ya Tanzania imeagiza ndege mpya ya biashara

Na hizo Sherehe za kupokea Ndege Airport pia huwa kuna kipigo cha hali ya chini.
Omba Mungu akusaidie upate nafasi ya kuzipiga Kodi zetu,kuumia au kulaumu ni matumizi mabaya ya akili yako. Jukumu lako ni kulipa Kodi matumizi yake sio jukumu lako
 
Acheni ndege zikuje, Simba na Yanga zitapewa bure kwenda Cairo na Jozi kuwakilisha Taifa.
 
Ni kweli, ndege ya pili aina ya B737-9Max inaweza kukabidhiwa kwa ATCL wakati wowote ingawa imechelewa.

B787-8 moja tangu mwaka jana iko parking Malaysia. Bombardier Q300 Iko parking Malta, wakati Airbus 220-300 ni moja au mbili tu zinazofanya kazi iliyokusudiwa, nyingine ziko parking au matengenezoni.

Najiuliza tu kama tuna kazi ya kununua ndege zifike hadi mia huku zikitumika zaidi kwenye ziara za viongozi ughaibuni? 😲
wangekarabati na viwanja vya ndege,kununua ndege bila ukarabati ni sawa na kununua mkoti wakati shati limechanika
 
Wiki ijayo tunapokea ndege nyingine ya fedha nyingi sana ambayo itaungana na ndege zingine za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Ununuzi wa ndege za mabilioni si tatizo, tatizo ni pale tumeruka hatua muhimu. Tulipaswa kutatua masuala ya maji, umeme, elimu, na afya kwanza kabla ya kufikiria kununua ndege.

Inafika wakati ambapo viongozi na waalikwa katika sherehe za kupokea ndege wanafananishwa na watu wasio na akili. Shule nyingi zina madarasa yanayoonekana kama maghala au mabanda ya kuhifadhi mkaa.

Vyoo na madarasa ambayo serikali inajivunia mtandaoni ni msaada wa COVID-19. Ni vipi tunafanya mambo muhimu kwa msaada halafu pesa zetu zinanunua ndege za mabilioni?

Choo cha shule kinajengwa kwa msaada. Je, unajenga choo kwa msaada na bado unataka sifa mara tatu? Leo hii, matibabu ya wazee na watoto ni bure lakini wanapata tu vipimo na wanapewa Panadol na Aluu, halafu wanatakiwa kununua dawa nyingine dukani.

Hali hii itaendelea hadi lini?

Kwa sasa, tuache masuala ya ndege kwa mashirika binafsi. Tutatue kwanza suala la vyoo shuleni na katika zahanati. Kuna choo kimoja karibu na mahakama, kinafunguliwa na msimamizi, ukiona unahitaji kwenda, lazima ulipe.

Bei ya Boeing 737-9 Max sokoni ni kubwa sana. Fedha hizo zingeweza kutumika kujenga madarasa ya kisasa bila kikomo. Watoto wakiwa darasani, wanaweza kufikiria wako chooni. Madarasa ni mabovu, na ofisi za walimu katika shule za umma zina mashimo ya kutosha.
View attachment 2942533
Hatuagizi mkuu hiyo ni danganya toto, yule kiongozi wa "MALAIKA" ndo aliweka order, hivo lazima tuichulue baba, sasa kwasababu tulizonazo zinatushinda na tunaziendesha kwa hasara.... kwanini hii tusimpelekee huko?!!!!
 
Wewe kuumia moyo haitasaidia kitu.

Na hakuna wakumlaumu zaidi yako mwenyewe, actually sisi wananchi wajinga,

Ngoja nikuambie kitu.

Watanzania kukosa maji au matibabu au hata msosi hiyo ni jambo la kawaida.

Watanzania wameishi maisha ya shida angali wakiwa wadogo na wamezoea hivyo kwahiyo kukosa hizo huduma ulizosema kamwe haziwezi kutushtua.

Hao unaowaita viongozi ni upande mmoja tu.

Ukitaka kumpata mtu wakumlaumu ingia chumbani kwako tazama kwenye kioo. Utamwona.
Kweli kabisa....🙆🙆🙆🙆
 
Wiki ijayo tunapokea ndege nyingine ya fedha nyingi sana ambayo itaungana na ndege zingine za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Ununuzi wa ndege za mabilioni si tatizo, tatizo ni pale tumeruka hatua muhimu. Tulipaswa kutatua masuala ya maji, umeme, elimu, na afya kwanza kabla ya kufikiria kununua ndege.

Inafika wakati ambapo viongozi na waalikwa katika sherehe za kupokea ndege wanafananishwa na watu wasio na akili. Shule nyingi zina madarasa yanayoonekana kama maghala au mabanda ya kuhifadhi mkaa.

Vyoo na madarasa ambayo serikali inajivunia mtandaoni ni msaada wa COVID-19. Ni vipi tunafanya mambo muhimu kwa msaada halafu pesa zetu zinanunua ndege za mabilioni?

Choo cha shule kinajengwa kwa msaada. Je, unajenga choo kwa msaada na bado unataka sifa mara tatu? Leo hii, matibabu ya wazee na watoto ni bure lakini wanapata tu vipimo na wanapewa Panadol na Aluu, halafu wanatakiwa kununua dawa nyingine dukani.

Hali hii itaendelea hadi lini?

Kwa sasa, tuache masuala ya ndege kwa mashirika binafsi. Tutatue kwanza suala la vyoo shuleni na katika zahanati. Kuna choo kimoja karibu na mahakama, kinafunguliwa na msimamizi, ukiona unahitaji kwenda, lazima ulipe.

Bei ya Boeing 737-9 Max sokoni ni kubwa sana. Fedha hizo zingeweza kutumika kujenga madarasa ya kisasa bila kikomo. Watoto wakiwa darasani, wanaweza kufikiria wako chooni. Madarasa ni mabovu, na ofisi za walimu katika shule za umma zina mashimo ya kutosha.
View attachment 2942533
Halafu ndege yenyewe Boeing 737-9 Max hata bure sipandi.
 
Ni afadhali wanunue maboeing hayo kuliko wakigawana pesa hizo kama posho za wao kuhudhuria makongamano, semina, vikao na warsha zisizojulikana
 
Hiyo mikataba alishasaini yule mbwa aliyekufa na akala cha juu,tuko katika utekelezaji tu, SSH wala asilaumiwe
Aliyeandika post hii yuko kama vile ni mtoto mbweha ndiyo maana anaonyesha chuki dhidi ya mbwa.
 
Mkuu Mimi naona serikali wako sahihi,

Kwasababu nyanja ya kiuchumi ndio inayoibeba/inayoiwezesha nyanja ya kijamii.

Ukiangalia katika muktadha wa kipaumbele kati ya kuwezesha/uwekezaji kati ya nyanja ya kijamii(elimu, afya, maji,nk) na nyanja ya kiuchumi(uwekezaji sekta ya usafirishaji, kilimo, madini, viwanda biashara nk.) utakua umefanya jambo la maana sana kama nguvu kubwa utaiwekeza kwenye nyanja ya uchumi kwani faida/matunda yatakayopatikana ndio yatasaidia kuimarisha na kuendeleza mambo/miradi ya kijamii.

Hata hivyo selikali inafanya mambo yote kwa pamoja kila nyanja imepewa nafasi kulingana na umuhimu/uhitaji/kipaumbele.
Wiki ijayo tunapokea ndege nyingine ya fedha nyingi sana ambayo itaungana na ndege zingine za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Ununuzi wa ndege za mabilioni si tatizo, tatizo ni pale tumeruka hatua muhimu. Tulipaswa kutatua masuala ya maji, umeme, elimu, na afya kwanza kabla ya kufikiria kununua ndege.

Inafika wakati ambapo viongozi na waalikwa katika sherehe za kupokea ndege wanafananishwa na watu wasio na akili. Shule nyingi zina madarasa yanayoonekana kama maghala au mabanda ya kuhifadhi mkaa.

Vyoo na madarasa ambayo serikali inajivunia mtandaoni ni msaada wa COVID-19. Ni vipi tunafanya mambo muhimu kwa msaada halafu pesa zetu zinanunua ndege za mabilioni?

Choo cha shule kinajengwa kwa msaada. Je, unajenga choo kwa msaada na bado unataka sifa mara tatu? Leo hii, matibabu ya wazee na watoto ni bure lakini wanapata tu vipimo na wanapewa Panadol na Aluu, halafu wanatakiwa kununua dawa nyingine dukani.

Hali hii itaendelea hadi lini?

Kwa sasa, tuache masuala ya ndege kwa mashirika binafsi. Tutatue kwanza suala la vyoo shuleni na katika zahanati. Kuna choo kimoja karibu na mahakama, kinafunguliwa na msimamizi, ukiona unahitaji kwenda, lazima ulipe.

Bei ya Boeing 737-9 Max sokoni ni kubwa sana. Fedha hizo zingeweza kutumika kujenga madarasa ya kisasa bila kikomo. Watoto wakiwa darasani, wanaweza kufikiria wako chooni. Madarasa ni mabovu, na ofisi za walimu katika shule za umma zina mashimo ya kutosha.
View attachment 2942533
 
Hukumsikia Bashungwa akitoa taarifa ya ukarabati wa viwanja vya ndege? Vyote viumefikia asilimia 80. Musoma,Dodoma, Mwanza. Baada ya hapo mtapanda ndege hadi mchoke.

Nchi hii usiwaamini wewe sikiliza kisha tambaa zako.
 
Mbona huumii serikali inapojenga barabara, tena barabara za ndanindani huko,

Au kwa sababu unajua kuna mtanzania atakutumia, hata kama serikali haitopata faida, ila kuna mtanzania atanufaika either kwa kupita au kupitisha gari yake, au kupitisha mazao yake.

Ili usiumie kwenye suala la ndege then Fanya assumption ya Aina hiyo, hata kama wewe hautopanda, ila kuna mtanzania ataipanda au atasafirsha bidhaa yake, au ataajiriwa kuihudunia hiyo ndege.

So, hizi zote ni namna ya serikali kusogeza huduma kwa jamii, ni the same na kujenga barabara au hospitali, lazima kuna mtu ataajiriwa kuihudunia na lazima kuna mtu itamfaa,

Ukiweza hivo then hutaumia.

Ila ukiwa na roho ya ubinafsi utaumia kila siku, ukisikia wamejenga daraja la busisi utaumia, ukisikia wamejenga barabara ya songea utaumia, ukisikia wamejenga uwanja wa mpira utaumia..... The list go on and on as long as haikugusi wewe itaendelea kuumia
 
Back
Top Bottom