Samia atosha tukutane2030
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 17,728
- 49,762
Mimi naishi Mvuti, ni mbali kidogo mpaka kufika mjini ila barabara yote ni mkeka mpaka mjini ninakofanyia kazi.
Barabarani nimeona sana damu za bodaboda na abiria wao.
Ukiona watu wamezunguka na mtu kafunikwa mtandio tayari aidha bodaboda au abiria wake hana uhai.
Siku moja niliona utumbo wa mrembo mmoja umemwagika kwenye rami 😭😭.
Madereva wa daladala hawana huruma kabisa. Wanaua bodaboda kwa makusudi kabisa wakijua bodaboda ni kundi lisilo na mtetezi.
Nimepanda bodaboda mjini mara nyingi, yatosha. Nimepona sasa siwezi tena kufanyia betting uhai wangu kwa kupanda bodaboda barabara kuu za Dar es salaam.
Sio tu bodaboda wanaokufa hata wale wanaotumia pikipiki zao binafsi kwenda kazini tumewazika sana. Kijana mmoja Daktari kafa mbichi kabisa pale TAZARA alikuwa akienda kazini Mloganzila.
Maisha hayana haraka. Tupande daladala, Mungu akikubariki nunua hata kigari used. Sasa hivi vigari namba B na C bei ndogo sana na mengine ni mazima kabisa.
Bodaboda wanakufa kama nzi. Mchana umemwona jioni tayari.
Bodaboda mlioko humu jf angalieni kazi nyingine, Familia bado zinawapenda hata kama serikali haiwathamini.
Mwangalie mke wako, waangalie watoto wako halafu imagine unafanya betting ya uhai wako kwa kichwa cha buku, buku jero, buku mbili.