Car4Sale Ninauza Coaster Used Safi (13M!)

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,186
Reaction score
7,492
Wakuu,

Ninauza Coaster Bus safi inafanya kazi ya daladala kati ya Temeke na Muhimbili. Gari ipo vizuri kama inavyoonekana katika picha na ipo barabarani inaendelea na kazi. Bei ni Mil. 13. Mazungumzo yapo kwa hiyo kama upo serious njoo tuzungumze. Kwa mawasiliano piga 0657457971 au 0685247148 (msimamizi wa gari). Karibuni sana wakuu gari ipo sokoni!
 

Attachments

  • coaster 1.jpg
    325.9 KB · Views: 72
  • coaster 04.jpg
    152.9 KB · Views: 59
  • coaster 08.jpg
    34.1 KB · Views: 64
  • coaster 02.jpg
    253.3 KB · Views: 62
ukitaka kuiona gari wasiliana na namba hapo juu, unaweza kuiona kati ya temeke na muhimbili muda wowote kati ya saa 12 asubuhi hadi saa mbili usiku.
 
8M unachukua mkuu?
Dah mkuu, hiyo hela kubwa hasa kipindi hiki cha Tanzania ya viwanda lakini kwa thamani ya gari yenyewe utakuwa umenibana sana mkuu. ongeza ongeza mkuu angalau ufikishe 12. tunaweza kufikia point nzuri.
 
Hiyo picha ni baada yakutoka garage kupigwa rangi eti mkuu?
 
Nimepiga mahesabu hiyo gari imeingia kwenye 2010! Miaka sita si haba. Mmeshatengeneza pesa ya kutosha kwa hiyo gari. Chukua hiyo nane na mwenzenu akaanzie maisha... Acheni tamaaa.
 
Shikamo dalali natafuta chumba sinza vipi nitapata?
Mkuu, kulingana na 'simulizi za mwenye kaya', Sinza sasa hivi vyumba ni bwerere. C unajua Sinza viwanda vimehama? Wapangaji wanafuata viwanda bhana. Viwanda sasa vimehamia Kibaha...
 
ukitaka kuiona gari wasiliana na namba hapo juu, unaweza kuiona kati ya temeke na muhimbili muda wowote kati ya saa 12 asubuhi hadi saa mbili usiku.

Mkuu naona tangu Zitto aliwe kichwa Chadema siasa zimekushinda umeamua kuwa Dalali.
 
Nimepiga mahesabu hiyo gari imeingia kwenye 2010! Miaka sita si haba. Mmeshatengeneza pesa ya kutosha kwa hiyo gari. Chukua hiyo nane na mwenzenu akaanzie maisha... Acheni tamaaa.
Wakati wewe unataka 8, wenzako wanasema lazima itakuwa ni mbovu maana m13 ni ndogo sana. Wanadamu tuna kazi kweli kweli.
 
Wakuu, Gari ishanunuliwa. Nawashukuruni nyote.
Shukran sana.
 
Costa au civilian nissan hyo mkuu!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…