Ninavyodhibiti gharama za umeme

Ninavyodhibiti gharama za umeme

Umeme ni moja ya gharama inayokula fedha sana,kwa sasa kwakuwa nimestaafu nipo home,natumia mbinu zifuatazo kupunguza matumizi ya umeme:

1.Kwenye nyumba nayoishi na mrs na familia kuna ststem mbili za umeme,wa tanesco na sola.Taa za kwenye geti na fensi natumia sola ambazo hujiwasha kuanzia saa 12 jioni,au giza likiingia

2.Umeme wa tanasco nautumia kwa taa za ndani,kuwezesha mafriji na vyombo vingine vya kupigia,tv,sistemu za muziki n.k ambapo ikifika saa 3 usiku taa zote za umeme za ndani tunazima na kutumia sola

3.Kwa kupikia natumia gesi na umeme ambapo yale majiki ya umeme ya kizamani,yaani zile oven kubwa tu na zenye banners za kupikia,tumeacha kutumia na zimebaki mapambo,sasa tunatumia majiko ya infrared,air frier ya kilo 10,pressure cooker ya kilo 10,ambavyo hutumia umeme kidogo kwa kazi kubwa

4.Matumizi yaa unawasha pale tu unapotaka kutumia na ukimaliza matumizi unazima,siruhusu taa kuwashwa bila sababu,vyakula aina ya maharage tunapika kwa pressure cooker tu,kuoka,kuchoma,kukaanga,kupika wali,ugali,chapati tuna alternate ama gesi ama air frier au pressure cooker.

Sasa kwa hatua zote hizo kwa mwezi nalipa umeme wa 60,000
Acha kuteseka, tafuta hela. Badala ya kutafuta hela unapambana kuzima taa kwenye nyumba.
 
Acha kuteseka, tafuta hela. Badala ya kutafuta hela unapambana kuzima taa kwenye nyumba.
ha ha ha sasa kipato changu ni kidogo,hivyo nazima taa za uneme wa tanesco nawasha za sola,kuna ubaya?
 
Kupitia comment nashauri wataalamu wanaoandaa mitaala wawe wanakuja huku MITANDAONI kuangalia na kujionea product zao wanazozalisha.

Ni aibu tupu watu wanacomment kama hawana vichwa lakini pia mtu anapost comment unasoma na unabaki unajiuliza hivi hawa wanaojiita GREAT THINKERS WA JF ni akina nani haswa, maana wengi wa JF members wanaashiria ombwe kubwa la maarifa,uwezo mdogo wa kifikra na kiuchambuzi na ukosefu wa mbinu katika kuyatafakari na kuyaendea mambo.

Mtoa mada kongole kwako kwa kushare your life experience but get to know your dealing with black people/ half humans half animals(too many savage people in here)😄😄😄🙏
 
Kama umesitaafu na unaandika namba hii... bila shaka wewe ulikuwa polis. Siwezi kuamini kama kuna msitaafu wa kada nyingine mwenye ujasiri wa kuandika hivyo kwenye sehemu kama hii
Huyu jamaa limbukeni mambo ya umeme ya nyumbani kwake na makorokovo cooker analeta hapa jukwaani ..siku akinyimwa papuchi atafunguka km kawaida yake .. kweli kuna watu humu chaneli chenga.
 
Huyu jamaa limbukeni mambo ya umeme ya nyumbani kwake na makorokovo cooker analeta hapa jukwaani ..siku akinyimwa papuchi atafunguka km kawaida yake .. kweli kuna watu humu chaneli chenga.
Punguza hasira kajiongelea yeye na jinsi anabana matumizi hajakuongelea wewe na familia yako aisee
 
kabla ya hapo ilikuwa nalipa 120,000
Umeshapiga hesabu, gharama unazotumia upande mwingine ni shilingi ngapi? Maana hapa naona picha unayoijenga ni kwamba umesevu 120,000 - 60,000 = 60,000/-. Jaribu kupiga hesabu ya unayoyafanya kama mbadala wa kutumia umeme huko nako unatumia shilingi ngapi. Isije ukawa huko kwenye mbadala unatumia zaidi ya 60,000/-
 
Sawa naupokea ushauri
Pia jaribu kutumia gesi pekee kwenye kupikia na usitumie umeme kabisa isipokuwa kwenye mambo mengine kama friji, pasi na taa. Halafu uone gharama zinakuwa ndogo kiasi gani.
 
Back
Top Bottom