Ninavyoziangalia siasa zetu

Ninavyoziangalia siasa zetu

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,230
Kila siku ninapoamka nakuzitizama siasa zetu, huwa najiuliza swali moja kama kweli kama taifa bado tunahitaji kuendelea kuwa na wanasiasa wa aina hii tuliyonayo. Kiuhalisia kila kitu Tanzania kimesimama au kinasuasua lakini hakuna anayeonyesha kustuka badala yake wanasiasa wetu wametingwa na mazingaombwe yao dhidi ya watu wanaowaongoza.

Wanasiasa wetu wameweka mfumo wa kuaminiwa wao zaidi kuliko Mitizamo, Falsafa au Itikadi wanazozisimamia. Rahisi sana kumshambulia Mbowe, Kikwete, Lipumba au mwingine yeyote yule kibinafsi kuliko kushambulia vile wanavyoviamini kwa kuwa havipo!!

Wanasiasa wetu kwa vitendo vyao si waliberali, si wajamaa, wala si mabepari, bali ni vinyonga wanaobadilika kutokana na wapi walipo na wapi wanaposema au kutenda wayatendayo. Siasa zinazoendeshwa na watu wasiofahamika misimamo yao kwa dhahiri ni siasa za watapihatima na wala haziwezi kujenga nchi. Wafuasi wao ni wafuasi wa umaarufu wa mtu unaoweza kuwa umesababishwa na kitu chochote kile hata nje ya siasa, na wafuasi hao huwa hawalindi kile huyo shujaa wao anachokiamini bali wanalinda yule wanayemuani hata kama hawajui shujaa wao huyo anasimamia nini.

Huwa najiuliza kama kuna mahali hawa "Mashujaa" wameshawahi kusema ni nini wanakisimamia kwenye nyanja ya Elimu, Afya,Sera za Kimataifa, Ajira, Ardhi, Kilimo au hata biashara. Na mara zote malumbano yao hujikita kwenye matukio na wala si kwenye hoja yakinifu muktadha wa maendeleo ya nchi yetu. Nikifika hapa huwa nagundua kwamba kumbe nchi yetu inaendeshwa kwa kudra za mwenyezimungu na hali hiyo itadumu kwa miaka mingi ijayo.

Hizi ni siasa uchwara!!
 
Hili ni tatizo tulilo nalo kama taifa!
Tumekosa "permanent interest",hivyo,kila chama kuja na vipaumbele vyao.
Ni vyema kama taifa kukaa chini na kuchagua vipaumbele vipi kila chama kitakapo ingia madarakani kutekeleza hivyo kwanza.
 
Hili ni tatizo tulilo nalo kama taifa!
Tumekosa "permanent interest",hivyo,kila chama kuja na vipaumbele vyao.
Ni vyema kama taifa kukaa chini na kuchagua vipaumbele vipi kila chama kitakapo ingia madarakani kutekeleza hivyo kwanza.
Kwanza siku zote vipaumbele huwa havichaguliwi na jamii bali "viongozi" huongoza jamii kufikia kwenye vipaumbele. Ukiona jamii haina vipaumbele vinavyoeleweka ujue misingi iliyowekwa na viongozi wa jamii hiyo ni mibovu. Marekani kwa mfano ni viongozi ndiyo waliowaongoza watu wao kuweka kanuni za kujiongoza tofauti na zile zilizokuwa zinatakiwa na Uingereza zifuatwe. Na nikisema "viongozi" si lazima sana iwe ina maanisha wanasiasa!!
 
Kwanza siku zote vipaumbele huwa havichaguliwi na jamii bali "viongozi" huongoza jamii kufikia kwenye vipaumbele. Ukiona jamii haina vipaumbele vinavyoeleweka ujue misingi iliyowekwa na viongozi wa jamii hiyo ni mibovu. Marekani kwa mfano ni viongozi ndiyo waliowaongoza watu wao kuweka kanuni za kujiongoza tofauti na zile zilizokuwa zinatakiwa na Uingereza zifuatwe. Na nikisema "viongozi" si lazima sana iwe ina maanisha wanasiasa!!

Kigarama,
Viongozi wabovu na wasio na maono huzalishwa na Jamii husika{Kumbuka viongozi hutokana na watu kutoka jamii husika},hivyo ni lazima tujitazame kama jami,what is wrong with us!!
 
Last edited by a moderator:
Ninakubaliana nanyi mkuu Kigarama na mkuu Mpenda Yesu,

Hapa nadhani kuna mambo kadhaa yanayochangia,

1. Jamii.
Jamii/asilimia kubwa ya wakazi bado hawana elimu ya kutosha ya uraia, na kama wanayo bado hawajaelimika/kuitumia vyema/ipasavyo.

Hii husababisha kufanya mambo kwa mazoea, kujuana, kimzaha.Hata inapokuja kwenye kuchagua viongozi mengi hutokea, kuchagua viongozi kutokana na mmoja wa wanafamilia/ukoo alikuwa kiongozi(mf. baba, mama, shangazi, mjomba n.k).

Pili wanajamii kuhofia mabadiliko na hivyo kufanya mambo kwa mazoea.


2. Viongozi:
Viongozi wengi wanasiasa/na wale wasio wanasiasa kupuuzia mambo, mf. Kiongozi kwa kutambua wazi maslahi ya Taifa hili ni haya na yeye kufanya kinyume.

Nakosa maana ya maneno haya "to take advantage" ya ujinga(kutokufahamu) kwa wananchi.Hata pale penye kuhitaji hekima ndogo bado ulaghai utahusishwa.


3. Mfumo:
Kila chama kinasema kikishika hatamu kitafanya haya na haya, na chama tawala kama ambavyo 'kimeshafanya' ya kwake.

Iwapo tutakuwa na mfumo fulani(mf. kama wa nchi ya Marekani) yaani, ingawa kuna vipaumbele vya kila chama, lakini chama chochote kitashika uongozi vipaumbele vya Taifa vitaanza kutekelezwa yaani vile vya muda mfupi(short term) na vile vingine vya Chama husika vitafuata vikienda sambamba na vile vya muda mrefu(long term goals) katika kutekelezwa.

Pili, kuna kitu fulani huwa nikijiuliza..katika makampuni binafsi, mashirika tunapitisha Usaili(Interview) tukichambua sifa mbali mbali za watu, hasa tukiangalia viwango vya elimu na uzoefu. Lakini inapokuja kwenye viongozi wa Taifa(ngazi mbali mbali) vigezo vitakuwa ni
1. Awe Raia wa Tanzania
2. Awe na umri kadhaa
3. Asiwe na kosa/makosa ya jinai
4. AWE ANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA.
5. N.k


Sasa unajiuliza iwapo viongozi tunaowachagua hatutilii mkazo sana katika Elimu, tunategemea tupate viongozi gani? Kwa mfano hebu tazama Elimu ya watendaji wa mhimili mmoja(Bunge)!Ni aibu karibu au zaidi ya asilimia hamsini(50%) wawe na elimu ya msingi.
Ufikiri, Upana, Utatuzi wa mambo utakuwa mdogo tu.


Tatu, adhabu mbalimbali hasa kwa viongozi(hasa wanasiasa) wenye kurudisha maendeleo hupuuzwa, mf. kiongozi anapojiuzulu, anapoomba radhi ili hali ameleta hasara kwa Taifa, wananchi(Jamii) huridhika bila kujali kilicgopungua, hata katika chama husika viongozi kama hawa huendelea kushika hatamu mbali mbali!
Sasa wanasiasa wachanga(makinda/chipukizi) huiga mifano hii hii na kuiendeleza.


Hivyo, Jambo na 3 hapo juu hutegemea sana jambo namba 2 ambalo hutegemea jambo namba 1. Mambo haya matatu(niliyoyataja hapo juu) huchangia sana katika kubadilisha(kwa kusonga mbele) siasa ya nchi.
 
Last edited by a moderator:
hippocratessocrates kwa maelezo yako inaonyesha kwamba mbele yetu kuna giza kubwa sana la matumaini!!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu Kigarama, kwa kiasi kikubwa mfumo uliopo hapa nchini ni chanzo kikubwa, na inatoka viongozi wengi hapa nchini wanatokana na mfumo wa kuthishana. Na nina amini tunafahamu uwezo wa viongozi wetu, na hili ndio matokeo ya yote haya.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom