MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mtu mmoja ambaye ni family friend na Koffi Olomide aliniambia kuwa Mzee Koffi kwenye mkataba wake wa kazi kaweka kipengele cha kutoongeleana vibaya baada ya mkataba kufikia tamati au kuvunjwa.
Hii ilitokana na tukio la mwishoni mwa miaka ya 90 pale wanamuziki wake wote walivyomtoroka kabla ya show ya Dar es Salaam na kwenda kuunda kundi lao.
Mimi niliona kama vile ni kipengele cha kinoko ila kwa kadiri ninavyopata uzoefu kwenye biashara naona KOFFI yuko smart.
Mwaka jana wakati naagiza mzigo wangu kwenye kampuni fulani Nairobi yule kijana wa Sales nikawa simpati Watsapp ikabidi nimcheki boss wake. Yule boss akaniambia bila hata kumuuliza kuwa kwa sasa yule kijana hafanyi kazi tena na sisi kwa sababu tumemfukuza kazi baada ya kutumia pesa nyingi sana za kampuni kwenye kamari (betting).
Nilishangaa sana kwasababu kijana mwenyewe ni wale born again wenye vyeo kanisani kwao. Kwa miaka zaidi ya 10 niliyomfahamu alikuwa kanyooka kama rula kwenye maadili. Kubwa zaidi alikuwa ni baba wa familia ya mke na watoto wawili. Hiyo kamari mbona ghafla sana?
Baada ya miezi kadhaa ndo nikapokea ujumbe wa yule kijana kuwa kwa sasa ana kampuni yake inayofanya biashara kama ile ya boss wake wa zamani. Kuhusu kamari sio kweli ni hila tu za kuharibiana majina. Kutokana na huduma zake kuwa nzuri nikaamua kufanya kazi na huyu kijana.
Tafadhalini wakuu msiharibie vijana majina kisa tu wameamua kwenda kutafuta malisho mazuri. Sababu kuu mbili za watu kuacha kazi ni maslahi duni na uongozi wa hovyo wa kampuni/taasisi.
Utakuta kijana alikuwa anapiga kazi inayosaidia kampuni kuingiza mabilioni ila mshahara wake hata milioni haufiki... au labda lugha mbaya za boss.
Kama ukiona kijana ana manufaa kwa biashara yako mwongezee maslahi and treat them well.