Kibenje KK
JF-Expert Member
- May 28, 2016
- 270
- 391
Mara nyingi ni vyepesi kusikia watu wakilalamika kuwa nafanya kazi lakini pesa siioni, Nafanya biashara lakini sioni faida.
Moja ya tatizo kubwa ni kuwa watu wengi hatuna taratibu za kupanga Bajeti na kuweka Akiba. Leo Tujifunze juu ya Akiba.
Akiba ni kiasi cha fedha au kitu kinachowekwa kwa ajili ya matumizi ya baadae.
Matumizi haya ya baadae ni muhimu yawe na malengo ambayo mtu anahitaji kuyafikia baada ya muda fulani.
Hakikisha kila wakati unaweka akiba na jambo la pili muhimu ni kuhakikisha kua akiba yako inazalisha kila siku kwa maana ya kuwekeza sehemu ambayo akiba yako ina ulinzi.
Utauliza, “Nitapata wapi pesa ya kuweka akiba wakati natumia yote ninayopata?”
Majibu ni: ukipata dharura pesa ya kuitatua hua inapatikana lakini kwa vile akiba ni kitu cha hiari hupati lakini👇🏿
Akiba inaweza kupatikana sehemu moja ya uhakika nayo ni kupunguza matumizi yako.
Unaweza kupunguza matumizi kwa kutumia huduma mbadala wa zile unazotumia kwa sasa ambazo ni chanzo kikubwa cha matumizi yako na kinasababisha ukose akiba kama ifuatavyo;
Badala ya kwenda kazini kwa bodaboda kila siku tembea kama ni karibu mwendo wa dakika 30 ni kidogo sana pia utakua umefanya mazoezi ya mwili.
Badala ya tax tumia usafiri wa umma kwenda kwenye shughuli zako za kila siku.
Badala ya kula mgahawani kila wakati jenga utaratibu wa kujipikia wakati mwingine inakusaidia pia kula vitu fresh na salama, sio lazima kila ukila uwe na soda pembeni kuna kisukari.😄
Angalia kodi ya nyumba kuna haja gani ya kupanga nyumba ya gharama kubwa, gharama zinazo ambatana na hiyo nyumba upunguze inapofaa
Tafuta kila namna kuweka akiba na iwe uwekezaji wako wa kila ukipata kipato.
Njia nyingine ni kuongeza kipato chako kwa kufanya kazi Zaidi.
Angalizo matumizi yana tabia ya kupanda mara mbili au Zaidi ya ongezeko la kipato.
Je unaweza kukumbuka ni wakati gani haukua mgumu na pesa kua hadimu?
Usipoipanga Kesho yako iweje, Kesho yako itakupangia uweje.
Weka akiba, Wekeza.
Kwa Mafunzo ya Biashara na, Ufanisi na maendeleo Binafsi. Wasiliana nami.
#kelvinkibenje
#begood