Ninawezaje kujenga Tabia ya kuweka akiba?

Ninawezaje kujenga Tabia ya kuweka akiba?

Kibenje KK

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2016
Posts
270
Reaction score
391
Mara nyingi ni vyepesi kusikia watu wakilalamika kuwa nafanya kazi lakini pesa siioni, Nafanya biashara lakini sioni faida.

Moja ya tatizo kubwa ni kuwa watu wengi hatuna taratibu za kupanga Bajeti na kuweka Akiba. Leo Tujifunze juu ya Akiba.

Akiba ni kiasi cha fedha au kitu kinachowekwa kwa ajili ya matumizi ya baadae.

Matumizi haya ya baadae ni muhimu yawe na malengo ambayo mtu anahitaji kuyafikia baada ya muda fulani.

Hakikisha kila wakati unaweka akiba na jambo la pili muhimu ni kuhakikisha kua akiba yako inazalisha kila siku kwa maana ya kuwekeza sehemu ambayo akiba yako ina ulinzi.

Utauliza, “Nitapata wapi pesa ya kuweka akiba wakati natumia yote ninayopata?”

Majibu ni: ukipata dharura pesa ya kuitatua hua inapatikana lakini kwa vile akiba ni kitu cha hiari hupati lakini👇🏿

Akiba inaweza kupatikana sehemu moja ya uhakika nayo ni kupunguza matumizi yako.

Unaweza kupunguza matumizi kwa kutumia huduma mbadala wa zile unazotumia kwa sasa ambazo ni chanzo kikubwa cha matumizi yako na kinasababisha ukose akiba kama ifuatavyo;

Badala ya kwenda kazini kwa bodaboda kila siku tembea kama ni karibu mwendo wa dakika 30 ni kidogo sana pia utakua umefanya mazoezi ya mwili.

Badala ya tax tumia usafiri wa umma kwenda kwenye shughuli zako za kila siku.

Badala ya kula mgahawani kila wakati jenga utaratibu wa kujipikia wakati mwingine inakusaidia pia kula vitu fresh na salama, sio lazima kila ukila uwe na soda pembeni kuna kisukari.😄

Angalia kodi ya nyumba kuna haja gani ya kupanga nyumba ya gharama kubwa, gharama zinazo ambatana na hiyo nyumba upunguze inapofaa

Tafuta kila namna kuweka akiba na iwe uwekezaji wako wa kila ukipata kipato.

Njia nyingine ni kuongeza kipato chako kwa kufanya kazi Zaidi.

Angalizo matumizi yana tabia ya kupanda mara mbili au Zaidi ya ongezeko la kipato.

Je unaweza kukumbuka ni wakati gani haukua mgumu na pesa kua hadimu?

Usipoipanga Kesho yako iweje, Kesho yako itakupangia uweje.

Weka akiba, Wekeza.

Kwa Mafunzo ya Biashara na, Ufanisi na maendeleo Binafsi. Wasiliana nami.

#kelvinkibenje
#begood
 
Nimecheka sana aiseee unataka kufundishwa kuweka ela mkuu,a cha pombe, punguza umalaya, sali sana jifunze kutulia nymbn kuepuka mitoko ambayo ni un-neccesary itakusaidia.
 
If huwezi weka hela' mwenyewe niunge na vicoba wanawake wanafanya sana hii wakati sisi wanaume tunamalizia pesa bar.
 
Mtoa mada kaeleza vizuri ila hajatoa solution ya tatizo.

Saccoss
Vicoba
Michezo
Fixed accounts etc

Ni baadhi ya majibu.

Uwezo wa watu kusave upo tatizo unaweka pesa mpesa na simu unatembea nayo, ukipatwa na emergency kidogo tu na huna pesa kwa wakati huo unalazimika kufanya muamala au kuingia ATM mwisho wa siku savings huzioni na hakuna kusonga mbele upo palepale au unarudi nyuma.

Pia saving inahitaji discipline sana na malengo.

Unapoweka pesa saving iwekee malengo, siyo unajaza pesa bila kujua utazifanyia nini.

Una lengo la kujenga, weka akiba kulenga ujenzi, una lengo la kuanzisha biashara weka lengo la kuweka saving kupata mtaji, una malengo ya kuweka pesa zikutumikie weka saving zako sehemu ambayo unakula faida kila baada ya muda fulani.

Kuwa na sababu ya kuweka akiba.

Kwa lugha nyingine ipe akiba yako jina, either mtaji, ujenzi n.k

Nidhamu ya hali ya juu ndiyo msingi.
 
If huwezi weka ela mwenyewe niunge na vicoba...wanawake wanafanya sana hii wakati.ss wanaume tunamalizia pesa bar
Kutokua na nidhamu ya pesa, baadae ndo unaanza kulalamika ooh mshahara haukai. Biashara haikui
 
Hayo yote nimeyafanya. Tatizo wanawake aisee, nisipohonga najihisi kupatwa na changamoto ya upumuaji
Kati ya vitu vinamaliza sana pesa ni wanawake. Ni muhimu uoe.

Kama muda bado jifunze kubadili tabia. Hiyo ni tabia na inaweza kubadilika
 
Mtoa mada kaeleza vizuri ila hajatoa solution ya tatizo.

Saccoss
Vicoba
Michezo
Fixed accounts etc

Ni baadhi ya majibu.

Uwezo wa watu kusave upo tatizo unaweka pesa mpesa na simu unatembea nayo, ukipatwa na emergency kidogo tu na huna pesa kwa wakati huo unalazimika kufanya muamala au kuingia ATM mwisho wa siku savings huzioni na hakuna kusonga mbele upo palepale au unarudi nyuma.

Pia saving inahitaji discipline sana na malengo.

Unapoweka pesa saving iwekee malengo, siyo unajaza pesa bila kujua utazifanyia nini.

Una lengo la kujenga, weka akiba kulenga ujenzi, una lengo la kuanzisha biashara weka lengo la kuweka saving kupata mtaji, una malengo ya kuweka pesa zikutumikie weka saving zako sehemu ambayo unakula faida kila baada ya muda fulani.

Kuwa na sababu ya kuweka akiba.

Kwa lugha nyingine ipe akiba yako jina, either mtaji, ujenzi n.k

Nidhamu ya hali ya juu ndiyo msingi.
Asante sana. Hii imeshiba sana
 
Back
Top Bottom