MNFUMAKOLE
JF-Expert Member
- Nov 14, 2014
- 1,502
- 1,886
Maana ya neno "ninawi" walitohoa kutoka neno "ni,na" na nina alikuwa ni mungu mke wa sehemu ile. hivyo waliamua kuita ninawi wakitemea ulinzi kutoka kwa huyo mungu mke.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna Mungu mke tena?Maana ya neno "ninawi" walitohoa kutoka neno "ni,na" na nina alikuwa ni mungu mke wa sehemu ile. hivyo waliamua kuita ninawi wakitemea ulinzi kutoka kwa huyo mungu mke.
Bora wakuu mmeliweka sawa maana story ilianza kupambwa na speaker na redio ,mji wa viwanda. Sijajua kama na airport za kisasa zilikuwepo au lah, ngoja muanzisha mada aje adadavue kidogo.Kilichoko iraq ni mji wa Babuloni,makazi ya mfalme Nebkadreza.Ninawi ni Spain.
Hahahaa. Jina lako linanikumbusa malkia wa sheba aliyemtembelea Mfalme solomoni. Wewe ni mjukuu wake?Great history !!
Ahsante rosemarie, hayo umesoma wapi kwa sababu umesema kuwa ulikuwa unasoma Bible,biblia yangu haina hizo habari nyingine za maendeleo ya Ninawi
Asante sana kwa hili, nashangaa sana wale wanaosema hakuna MunguNinawi ni mji mkongwe na uliokuwa maarufu zaidi miaka ya Yona,mji huu unapatikana katika nchi ya Syria karibu kabisa na mji unaoitwa Mosul uliopo Iraq
Ninawi ulikuwa mji muhimu sana kwa sababu barabara ya kuelekea miji ya kusini na kaskazini ilikuwa inapita katikati ya ninawi
Vile vile kuna mto mkubwa unaitwa khawser unapita katikati ya ninawi na ulisaidia sana kukuwa haraka kwa mji kwa sababu ya kilimo kilichotegemea sana mto huu
Watu wa kwanza kuishi ninawi walikuwa wakiitwa Neolithic na walikuwa wakulima
Kwa nini Yona alikataa kwenda ninawi?
Ni siku ya tatu leo nasoma kitabu cha Yona na nimegundua mambo mengi sana ambayo Bibilia haikuweka wazi sana,Kwanza historia ya Ninawi na historia ya Yona
Ninawi ulikuwa ni mji mkubwa sana na tukirudi nyuma enzi za Nimrod Yule mtu aliyemuasi Mungu na kutaka kujenga mnara ili ufike Mbinguni aliishi mji ule,au ni kabila moja na wakaazi wa mji ule,
Yona alijua vizuri historia ya Ninawi na ndio maaana alipotumwa na Mungu kwenda kuhubiri alikimbilia mji mwingine Tarshishi ili kuuepuka mji ule mkubwa
Viwanda vilikuwepo ndani ya Ninawi enzi hizo na mji ulikuwa umejaa wasomi wa kila aina hata barabara zake zilikuwa hazina mfano kulinganisha na mahali popote pale duniani enzi hizo
Yona alikuwa Myahudi na alijua wazi watu wa ninawi walikuwa adui za wayahudi na adui wa Mungu
Alipopewa ujumbe kuelekea ninawi alikaa na kufikiri na kujipima na akaona hafai hata kidogo kwenda kupeleka ujumbe kwenye mji mkubwa wenye viwanda uliojengeka kiuchumi na uliojaa maelfu ya watu wasomi na walioitwa wastaarabu enzi hizo
Mungu anashangaza sana kumtuma mtu mmoja kwenye mji mkubwa kiasi hiki bila maspika makubwa wala kumtangaza kwenye tv na radio na wasaidizi kibao wakiambatana na mafundi mitambo!!!!!hiyo inashangaza
Nimemaliza kitabu cha Yona na nimeona vema kuwagawia nilichojifunza
Mungu awabariki!
View attachment 140523
Ninawi ni Spain na sio mashariki ya kati kwani huwezi kupanda boti,meli au jahazi toka syria kwenda Mosul,Iraq ni sawa na mtu aseme naenda dodoma na meli toka dar.Yona alitoka mashariki ya kati kwenda Spain (NINAWI)na alimezwa na nyangumi katika bahari ya Mediterenian.
Tuwatag wajeKwakuwa mnabishana mtoa mada unasema ninawi ulikuwa Middle east hapo mwingine anasema ninawi ilikuwa spain sasa wote subirini walioishi ninawi karne hizo Waje hapa
Ninawi ni mosul ya Leo.Ninawi ni mji mkongwe na uliokuwa maarufu zaidi miaka ya Yona,mji huu unapatikana katika nchi ya Syria karibu kabisa na mji unaoitwa Mosul uliopo Iraq