Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
Naona ushauri,
Kwa jina naitwa Yusrath Mohamed. Mimi ni Binti mwenye miaka 19 kwasasa.
Nyumbani kwetu sio matajiri na wala sio masikini bali ni maisha ya kawaida. Inshort mimi sio mtoto wa kishua.
Baba yangu ni mwajiriwa wa serikalini na mama yangu ni mama wa nyumbani. Mimi ni mtoto wa tatu kuzaliwa kati ya watoto watano kwenye familia yetu. Tupo waschana wawili, yupo dada yangu ambaye ni wa pili kuzaliwa na wakwanza kuzaliwa ni wa kiume na wa mwisho wawili ni wa kiume pia.
Katika familia yetu wote tumebahatika kupelekwa shule kaka na dada yangu wamefanikiwa kuhitimu hadi chuo kikuu na sasa nao wana kazi zao. Wadogo zangu wawili wapo sekondari lakini mimi nilihitimu tu kidato cha nne mwaka uliopita lakini sikufanikiwa kupata ufaulu mzuri wa kunipeleka kidato cha tano na sita bali nilipata ufaulu mdogo ambao unaniruhusu kwenda chuo kwa ngazi ya certificate hasa kwa kozi ya ualimu kama zilivyo ndoto zangu.
Nilipokuwa kidato cha tatu nilitokea kumpenda sana kaka yangu, mtoto wa mjomba wangu. Na hii ni kutokana na yeye kuonesha kuwa ni mtu anayenijali sana kwa vitu vingi kiasi cha mimi kuvutiwa nae na nikajikuta nafall in love kwake. Nia na matamanio yangu ni kuolewa na yeye.
Najua unaweza ukashangaa lakini sisi kwa mujibu wa dini yetu ya kiislamu hasa huku Zanzibar inaruhusiwa kabisa kuoana na mtoto wa mjomba au wa shangazi na hakuna shida. Hiki ndicho kitu ambacho huwa kinanipa moyo siku zote na kuamini kuwa pengine ndoto zikatimia.
Kwakweli ni mtu mwenye kujali sana, sijui yeye anafanya vile kama ndugu au na yeye ana mapenzi na mimi.
Nimejitahidi kuonesha kila ishara kwake ili aweze kunitongoza nami nione hisia zake kwangu lakini imeshindikana. Mimi kama mwanamke nimeshindwa kumtamkia kama nampenda na nahitaji anioe lakini nimemfanyia kila kitu ili kumuonesha mapenzi yangu kwake.
Ninaposema nimemuonesha kila kitu simaanishi labda nimewahi kulala nae kimapenzi hapana bali ni ile mitego ya kimahaba ambayo ukimfanyia mtu ni lazima tu atakuwa na hisia fulani na kuona kuwa unamuhitaji kimapenzi.
Huku Zanzibar kulala kimapenzi na mwanaume ambaye sio mume wako ni kitendo cha ajabu sana. Kwanza ni dhambi lakini pia ni kitendo kinachoweza kuidharirisha familia yako. Lakini pia baba yangu ni mkali mno niliogopa akijua angeweza kunipiga sana, ukizingatia baba yangu ni kiongozi mzuri wa dini.
Hivyo hata mimi pamoja na mitego yote lakini sikuwa kulala nae japo nilikuwa napenda sana kwenda kwao na wakati mwingine tunakuwa tu wawili nyumba nzima wazazi wanakuwa hawapo nyumbani na yeye pia alikuwa akipenda kuja kwetu.
Nikiwa nasubiri labda kuna siku atanitamkia kuwa anahitaji kuwa na mimi, nilikuja kusikia kuwa ana mahusiano na msichana mwingine na yupo mbioni kuoana nae. Dah! Aisee niliumia sana. Siku ya kwanza mimi kupata taarifa hiyo nilijifungia ndani na kulia mno. Nikiulizwa nalilia nini najibu kichwa kinauma na nikipewa dawa nazitupa uvunguni mwa kitanda.
Lakini sijui kilitokea nini, yule mchumba wake alikuja kuolewa na mtu mwingine. Hapo nilihisi sasa ndio wakati wa yeye kuwa na nia na mimi lakini haikuwa hivyo.
Nikiendelea kukasirika sana n kuhisi labda ananidharu au anaona mimi sifai kuolewa na yeye. Lakini nikijiangalia naona mbona mimi ni mzuri kuliko waschana wengi hapa mtaani na pia ni bikra sijawahi kutembea na mwanaume yoyote tangu nizaliwe sasa kwanini yeye haoneshi kuwa na hisia na mimi! Inaumiza sana.
Basi niliamua nianze kumpotezea na kila akija nyumbani najifanya sipo, najifungia tu chumbani na hata nikiitwa nitoke nje sitoki.
Kuna siku baba alituambia kuwa kuna kikao kwa Mzee fulani ambaye pia ni ndugu upande wa baba. Familia yote ilienda lakini mimi na mama hatukwenda tulienda shamba.
Baba alivyorudi akamwambia mama kuwa kuna mtu anataka kunioa hivyo mama aongee na mimi na kama nikiwa tayari basi wamruhusu aendelee na taratibu nyingine za kukamilisha swala zima la ndoa.
Mama alipokuja kuniambia, nikamkatalia nikasema sipo tayari kuolewa kwasasa. Lakini mama aliniambia
"wewe ni mkubwa sasa, kama shule umeshamaliza hivyo kuendelea kubaki nyumbani ni kutudharirisha wazazi wako na hata baba yako nikimwambia kuwa hutaki kuolewa atakasirika sana pia ataona umeamua kumdharau. Usifanye hivyo mwanangu."
Nikiwa naendelea na mazungumzo na mama, simu ya dada ikaita. Siku hiyo nae alikuwa nyumbani kumbe ni mtoto wa mjomba mwingine ndiye aliyekuwa anataka kunioa lakini bado katika mazungumzo yetu na mama hatukufikia hadi kuniambia ni nani anayetaka kunioa.
Dada akaniita na kuniambia fulani anataka kuongea na wewe, lakini alivyonitajia jina nikakataa kuongea nae kwani yeye sio mwanaume ninayempenda. Tangu mwanaume niliyempenda mimi kuonesha kutonihitaji basi nikachukia sana na kuona siwezi kuolewa na mtu mwingine tofauti na yule nimpendae kwa dhati tangu nilipokuwa shule hadi sasa.
Dada alinilazimisha na hatimae nikakubali kuongea nae ndipo aliponieleza kuwa anahitaji kunioa na teyari ameshawaambia wakubwa siku ile ya kikao lakini nikamjibu kuwa sitaki kisha nikarudisha simu kwa dada.
Nikarudi kuendelea kuongea na mama, mama nae alinitajia mtu yuleyule kuwa ameonesha nia ya kutaka kunioa.
Kwakuwa sikuwa tayari nikaamua kumwambia mama kuwa nina mchumba wangu ambaye tupo tayari pia kunioa ili wasije kunilazimisha niolewe na huyo aliyejitokeza kutaka kunioa. Kwa ninavyomjua baba na ukali wake ni lazima angenilazimisha.
Wazazi walitaka basi kama nina mchumba nimwambie ajitokeze nyumbani ili tuone kama ana nia kweli ya kutaka kunioa lakini kama hayupo tayari kujitokeza basi ni lazima nikubali kuolewa na huyu aliyejitokeza ili kuistiri familia kuliko kuzeekea nyumbani.
Hazikupita siku nyingi yule mtoto wa mjomba niliyempenda mimi akapa mchumba mwingine na akaoana nae. Mimi nilizidi kuchanganyikiwa na kuona malengo yangu hayatoweza kutimia tena. Huku yule mtoto wa mjomba mwingine akawa anaendelea kunitafuta na nia yake hiyohiyo ya kutaka kunioa basi nikaona tu nikubali kuolewa nae hivyohivyo japo moyoni mwangu yupo mtu mwingine nimpendae kuliko chochote lakini ndio hivyo nae ameshaoa.
Nilivyokubali alijitokeza rasmi nyumbani akalipa mahari na hivi karibuni tutafunga ndoa inshallah. Lakini bado moyo wangu unaniuma sana. Huyu sijampenda.
Kuna muda namfanyia vituko vingi ili aniache lakini ananiomba msamaha hatakama kosa nimefanya mimi. Huyu ananijali kwa kila kitu na hakika naweza kusema ananipenda sana. Kama ningekuwa nampenda basi ningesema nimepata bahati lakini kiukweli simpendi ila nimekubali tu kishingo upande, yani basi tu nifanyeje.
Mimi nampenda yule aliyeoa japo sijawahi kumwambia kama nampenda na pia sijamwambia mtu yeyote siri hii, wewe ndio mtu wa kwanza kukupa siri hii naomba unishauri nifanye nini.
Lakini pia, je kama mwanamke eti ni sahihi kutamka hisia zangu kwa mtu ninayempenda?
Naomba ushauri wako tafadhali au nipostie katika page zako nitasoma comments.
@Yusrath Mohamed - Mji Mkongwe Zanzibar"
_______________
NB: Hii sio simulizi bali ni ujumbe kutoka inbox yangu na ni kisa cha kweli. So please! ushauri wako ni muhimu.
It's me
A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
Office Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com