Habari zenu? Kuna single mama mmoja binti wa miaka 25, nimekuwa naye kwenye mahusiano Kwa karibu mwaka mmoja na sasa hivi ana ujauzito wangu wa miezi 5. Ila ana mtoto wa miaka mitano aliyezaa na mwanaume mwingine. Huyo mwanaume walishaachana kitambo tangu mtoto akiwa ana mwaka na jamaa huwa anatuma fedha za matumuzi tu.
Sasa Mimi nikawa nimevitiwa na huyo dada kutokana na uchapakazi wake, na hata dukani ana kauli NZURI Kwa wateja na ana mkono wa Biashara kweli kweli. Nikaona huyu ndiye mwanamke wa kuanza naye maisha japo nawaogopa ma single mother ila nikaamua Nile ngumu.
Cha ajabu majuzi nimekuta msg za mwanaume mwingine kwenye simu, Tena sio baba mtoto wake ila mwanaume mwingine kabisa na walikuwa wnapanga miadi ya kuonana waka vunje amri ya sita. Sasa kilichonishitua zaidi ni binti huyu kuwa na uthibutu wa kuchepuka akiwa mjamzito Tena Tumbo tayari limeanza kuonekana. Hivi akishajifingua itakuwaje?
Sasa hapa niko dilema sijui nifanyaje coz ujauzito ni kweli WA kwangu Nina uhakika asilimia 98, na binti ni mchapa kazi Yana ana sifa zote za kuwa mke. Ila kilichonishitua ni hiyo tabia yake. Najiuliza kama itakuwa sahihi kumuacha akiwa mjamzito?
Na pia nilipomuuliza kuhusu huyo MCHEPUKO alijotetea akasema ilikuwa ni chatting tu, coz ni mwanaume wake wa zamani sana ila hawajafanya chochote, na ameshamwambia kuwa yeye ni mchumba WA mtu hivyo hakuna kinacho endelea kati yao.
Mnanishaurije hapo wadau?
1petro3.7
"Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili" ✍️
Me nawashangaa sana vijana wanaokimbilia kuoa eti kwasababu wanao uwezo wa pay bills na mahitaji mengine kwa mwanamke so sadness 😢
Ni wanawake wangapi tunashuhudia kwake kuna kila kitu hakosi chochote na gari kanunuliwa lakini anatoka nje ya NDOA yake na dereva bodaboda
Kijana Pesa, magari, na mali sio hitaji la kwanza kwa mwanamke na ukimtangulizia mwanamke hivyo vitu umekwisha takakuja akufanye kitu kibaya sana hata ikapelekea kumtenda ubaya na kuishia jera
Hitaji la kwanza kwa mwanamke ni kumfanya awe Bora na hili ndo hitaji muhimu na kubwa kwa mwanamke yoyote
Kitu ambacho wengi hawajui hata wanawake wenyewe hawajui hi Siri ni kwamba MUNGU ameweka kila kitu NDANI ya MWANAMKE, kuna hadhina kubwa sana NDANI ya MWANAMKE yoyote kwa familia na ndoa yake ila tatizo Wengi hawajui jinsi ya kudispay hi hadhina kwa NDOA, familia Hadi katika jamii inayowazunguka
Kizazi cha Leo cha jinsia ya kike kilivyopotoka na kukosa maarifa eti unakuta MWANAMKE anatafuta MTU mwenye Pesa au KAZI au tajiri ndo aolewe nae 😢..... Wakati hivi vyote hawafahamu kua MUNGU ameviweka NDANI yao kwaajili ya familia na NDOA zao
Kijana
mke katika NDOA utampata ukiwa huna kitu chochote Kwaiyo tafuta Mwanamke ambae atakuvumilia ukiwa zero wapo wengi na huyo ndiye mke bora, ...
Ukitaka kupata
Mwanamke katika NDOA we tafuta binti ukiwa tayari na kitu mkononi hawa viumbe wanaongozwa na tamaa afu ngojea itokee siku hicho kitu kimeondoka ndo utamuona sura yake
KUNA TOFAUTI KATI YA MKE NA MWANAMKE ,
👉AKILI ITAMBADILISHA MWANAMKE KUA MKE B'SE UNAPOKUTANA NA BINTI AT FIRST TIME HUYO NI MWANAMKE SASA NI JUKUMU LAKO KIJANA KUMBADILISHA HUYO MWANAMKE KUA MKE NA SIO KAZI NYEPESI HATA KIDOGO INAHITAJI HEKIMA NA AKILI
MWANAUME Ukitaka kuona dunia chungu na upoteze Radha ya MAISHA ya hapa duniani oa kiumbe kinachoitwa MWANAMKE ndo utaona shughuli yake
Na hapa ndo utaukumbuka ule msemo wa kiswahili usemao "
kosea vitu vyotee..! ila usikosee kuoa"😀
Niwaibieni Siri wana mama na dada zangu👉 MWANAUME anaekupenda ni yule anaekufanya wewe uwe BORA na si yule anaekupa vitu ✍️