Ninayetaka kumuoa ana mchepuko mwingine

Ninayetaka kumuoa ana mchepuko mwingine

Habari zenu? Kuna single mama mmoja binti wa miaka 25, nimekuwa naye kwenye mahusiano Kwa karibu mwaka mmoja na sasa hivi ana ujauzito wangu wa miezi 5. Ila ana mtoto wa miaka mitano aliyezaa na mwanaume mwingine. Huyo mwanaume walishaachana kitambo tangu mtoto akiwa ana mwaka na jamaa huwa anatuma fedha za matumuzi tu.

Sasa Mimi nikawa nimevitiwa na huyo dada kutokana na uchapakazi wake, na hata dukani ana kauli NZURI Kwa wateja na ana mkono wa Biashara kweli kweli. Nikaona huyu ndiye mwanamke wa kuanza naye maisha japo nawaogopa ma single mother ila nikaamua Nile ngumu.

Cha ajabu majuzi nimekuta msg za mwanaume mwingine kwenye simu, Tena sio baba mtoto wake ila mwanaume mwingine kabisa na walikuwa wnapanga miadi ya kuonana waka vunje amri ya sita. Sasa kilichonishitua zaidi ni binti huyu kuwa na uthibutu wa kuchepuka akiwa mjamzito Tena Tumbo tayari limeanza kuonekana. Hivi akishajifingua itakuwaje?

Sasa hapa niko dilema sijui nifanyaje coz ujauzito ni kweli WA kwangu Nina uhakika asilimia 98, na binti ni mchapa kazi Yana ana sifa zote za kuwa mke. Ila kilichonishitua ni hiyo tabia yake. Najiuliza kama itakuwa sahihi kumuacha akiwa mjamzito?

Na pia nilipomuuliza kuhusu huyo MCHEPUKO alijotetea akasema ilikuwa ni chatting tu, coz ni mwanaume wake wa zamani sana ila hawajafanya chochote, na ameshamwambia kuwa yeye ni mchumba WA mtu hivyo hakuna kinacho endelea kati yao.

Mnanishaurije hapo wadau?
Yani unagongewa bado unakuja kuomba ushauri...acha uboya
 
Sikiliza moyo wako.....kama moyo wako unasema muache....basi muache....kama moyo wako hautaki kumuacha, sisi hata tukishauri haisaidii...muamuzi wa mwisho ni moyo wako
 
Kuna single mama mmoja binti wa miaka 25, nimekuwa naye kwenye mahusiano
Kanuni ni zilezile inapohusu single maza

●Hatulei bao la mwanaume mwingine

●Mwanaume anatakiwa aanzishe familia yake sio ajiunge kwenye familia ya mwanaume mwenzake

●Single maza waolewe na baba za watoto wao

●Single maza ni wa kupiga na kusepa

Ni mwanaume mpumbavu na mjinga tu ndiye anayeweza kumuoa single maza

Learn or perish
 
Kama mimba ni yako una uhakika jifanye hujaona maisha ya endelee mkuu kwani Kila mwanamke Ana kasoro zake

Huyu hajui kupika,huyu Malaya,huyu kitandani gogo,huyu hajui kuoga na yule ana mdomo

Ukitaka kudumu na mkeo kaambali na simu yake/na jifunze kuya tafuta mema yake sio mabaya yake utaishi nae kinyume na hapo uta kufa huna mke
Kwa kufa bila mke au mume ni dhambi? Wateule wa ndoa ni wachache mkuu.
 
Back
Top Bottom