Ninazuiwa kupata uhamisho kazini, nifanye nini?

Mrs minel

Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
65
Reaction score
54
Habari walimu wenzangu, najua mpo. Mimi nilifuatilia uhamisho direct mwenyew Tamisemi kwa Katibu Mkuu kutokana na changamoto za maradhi.

Nilitumia vyeti vya hospitali kumuomba Katibu Mkuu hatimaye akanipa kibali, sasa huku halmashauri kwangu Afisa Utumishi amegoma kunifungia data kuwa mpaka nilete nyaraka nilizotumia kuomba uhamisho Tamisemi.

Nifanyaje wadau?
 
Pole sana mwalimu, walimu wamekuwa wakipitia changamoto hizi yote hii ni kukubali kuwa mwalimu

nakushauri chukua mikopo benki 5 tofauti kusanya million 40 halafu tokomea kwenye biashara

utakuja kunishukuru

ACHANA NA UALIMU
Shida ni kuwa hakuna benki itakayompa mkopo ilhali ana mkopo benki nyingine zaidi ya mbili......labda achukue pesa za vicoba,saccos,kule kwao cwt,na mikopo nyonya damu mingi
 
Habari walimu wenzangu, najua mpo. Mimi nilifuatilia uhamisho direct mwenyew Tamisemi kwa Katibu Mkuu kutokana na changamoto za maradhi.

Nilitumia vyeti vya hospitali kumuomba Katibu Mkuu hatimaye akanipa kibali, sasa huku halmashauri kwangu Afisa Utumishi amegoma kunifungia data kuwa mpaka nilete nyaraka nilizotumia kuomba uhamisho Tamisemi.

Nifanyaje wadau?
Kuna athari gani endapo ukipeleka kopi za hizo nyaraka?
 
Yani Mimi nipewe kibali Cha uhamisho na katibu mkuu halafu nirudi kwa afisa utumishi kuomba ridhaa?anachopaswa afisa utumishi ni kukupangia kituo kipya fullstop,hana mamlaka ya kuzuia uhamisho wako,unless sielewi taratibu za uhamisho tamisemi,hao Maafisa utumishi wanajiona Miungu watu ndomana wengine wanashughulika nao kimafia🤣
 
Habari walimu wenzangu, najua mpo. Mimi nilifuatilia uhamisho direct mwenyew Tamisemi kwa Katibu Mkuu kutokana na changamoto za maradhi.

Nilitumia vyeti vya hospitali kumuomba Katibu Mkuu hatimaye akanipa kibali, sasa huku halmashauri kwangu Afisa Utumishi amegoma kunifungia data kuwa mpaka nilete nyaraka nilizotumia kuomba uhamisho Tamisemi.

Nifanyaje wadau?
Hilo ni jambo dogo sana, nenda kwa mzee wa Upako pale Ubungo na kesho yake utakuwa mtu mwenye furaha.
 
Anayekufungia Data sheet ni mkurugenzi sio Afisa utumishi

Nenda kwa mkurugenzi fatilia documents zako

Kama hataki rudi TAMISEMI uone kama hawatakupa.

And sasa wewe unasoma kama mtumishi wa huko unakoenda na sio hapo.

Shida wa Taasisi nyingi za Serikali zinanuka Rushwaa .

Hata huyo anataka rushwa

Hivi huku Hawkins TAMISEMI

Muone watu wanu wanavyotesekaa
 
Kuna Dada mmoja kapata barua toka tamisemi na wanakataa kufunga data sheet mana wamerejea kwenye file hawaoni mchakato wowote wa kuomba uhamisho.Nakushauri andika barua ya kuomba weka tarehe za zamani mhonge masijala akachomeke afu muone mkurugenzi
 
Pole sana

Kiutumishi HRO ana haki ya kufahamu ulipataje kibali cha uhamisho.
Punguza kutunisha misuli nahisi ndiyo ugomvi uliopo baina yako na huyo Hro wako.

Ila HRO wengi wa halmashauri zetu ni Incompetent so kuwa mpole muombe akusaidie tu
 
Hilo haliwezekani. Kumbuka barua inaanzia Kwa mkuu wa kituo, naye atakubali kubackdate?
 
Pole sana

Kiutumishi HRO ana haki ya kufahamu ulipataje kibali cha uhamisho.
Punguza kutunisha misuli nahisi ndiyo ugomvi uliopo baina yako na huyo Hro wako.

Ila HRO wengi wa halmashauri zetu ni Incompetent so kuwa mpole muombe akusaidie tu
Huu ndo ushauri, au amtafute mtu anayemmudu huyo HR ambembeleze aongee nae.
 
Back
Top Bottom