Ninetengwa na familia ,mke kanikimbia kisa message ya ushirikina

Ninetengwa na familia ,mke kanikimbia kisa message ya ushirikina

Kama ni kweli wana lao jambo hao sababu kama ni hizo msg mbona siku hizi zinatumwa sana tena sio mtu mmoja.

Pole sana ila liangalie kwa undani hilo swala sababu msg haiwezi kuwa chanzo cha yote hayo. Yaani mandishi tu ndio yazue seke seke lote hilo. Mmh.



Labda wamemtafutia sababu.


ila nikiangalia mwandiko wa mleta mada naona ni story ya kutunga. Kuonyesha hizi mesage zinavyoweza kuleta tafrani.

TCRA wakiwa wajanja walifanyie kazi maana ni kero.

Najiulizaga hizi mesage adi magufuli anazipataga kweli??
 
Labda wamemtafutia sababu.


ila nikiangalia mwandiko wa mleta mada naona ni story ya kutunga. Kuonyesha hizi mesage zinavyoweza kuleta tafrani.

TCRA wakiwa wajanja walifanyie kazi maana ni kero.

Najiulizaga hizi mesage adi magufuli anazipataga kweli??
Hata mie nimedhani hivyo kama usanii vile.

Na pia sidhani kama yule jamaa anazipataga sababu angekuwa anazipata hili swala lingeshafanyiwa kazi siku nyingi na wala isingekuwa tabia endelevu kiasi hiki yaani ingeshakufaga hii tabia ya hawa matapeli kutuma msg zisizo na kichwa wala miguu kila kukicha.
 
Hayo ma SMS ya kijinga watu huwa wanayatuma tu , we tulia akikaa huko kwao akichoka atarudi, wala usichukue maamuz magumu, it is just a matter of time.
Hizo sms huwa natumiwa karibu kila wiki na ni line zote.
Nadhani huenda huyo bibie aliishia darasa la pili au hakutaki alikuwa anatafuta sababu ya kuachana nawe!
 
Hawa watu ni washenzi, hata mimi mke wangu aliwahi kutumiwa sms za namba hii, mueleweshe mkeo
 
Kuna dalili ya kuwa huu uzi wa kutunga nani adiyeijua hiyo text?
 
Mke Wakoo katokaa KOLOMIJEE JANAA??? Kwelii ushambaa zigoo la mwibaa
 
Mke wako na ndugu zako ni Wapumbavu. Mshukuru mungu kwa kukuepusha nao
 
Nipo kwenye simanzi kubwa kwa takriban wiki 2 sasa familia ya mke imenitenga ,mke kanikimbia na baadhi ya ndugu zangu wamenitenga wakidai nimewaaibisha.

Siku ya tarehe 29 January mke wangu alichukua simu yangu na kuanza kupekua na mie huwa sina nongwa na huwa sifichi simu yangu siweki password yeyote sina tabia hizo sababu siwezi kufanya maujinga kwenye simu yangu.

Sasa shida imekuja mke wangu kakutana na sms ya mtu anayejifanya mganga na kiukweli Huyo mtu simjui na namba yake siifahamu kabisa ila sms yake inasomeka kama vile ananifahamu na tuliwahi kuonana ..sasa mke wangu kaanza vurugu na kunisema mimi mshirikina naenda kwa waganga ili nimroge atulie sijui simwamini na maneno kedekede kila nikijaribu kumweleza haelewi na ndugu wa mke na ndugu zangu wamepigiwa simu na kupewa malalamiko hayo kila nikijaribu kuwaelezea hawanielewi huku baadhi ya ndugu zangu wanadai nimewaaibisha ,


Wapo wanasema wanipeleke kwenye maombi nikaombewe binafsi nimekataa kila nikitaka kuwaelewesha hawataki kunielewa na siwezi kwenda kuombewa wakati ni sms ambayo binafsi sijui ni nani kaituma mpaka muda huu wamenitenga

Na hali ikiendelea hivi nimeamua kutoa maamuzi mazito juu ya familia yangu liwalo na liwe

978fd8a5fe0ec508fa71c4ed37e3ab86.jpg
Huyo mkeo ndio amekutumia hiyo message ili spate excuse ya kuachana na wewe...
 
Ukipata mesej kama hiyo kwanini usifute!? Ninapokua kwenye foleni kazi yangu Ndio hiyo kufuta mesej za mitandao ya simu na ambazo sizihitaji na kufuta Picha zinazojidownload au za magroup
Kuwa mpole wife atarudi mwenyewe au mpe iyo namba aipige aongee nae aone jinsi atakavyo sumbuliwa
 
Huyo mke mm naona ana mambo tu ya kitoto
Sasa je km angekuta meseji ya kugegedana c angezima na kufa kabsa
 
Back
Top Bottom