Nipo kwenye simanzi kubwa kwa takriban wiki 2 sasa familia ya mke imenitenga ,mke kanikimbia na baadhi ya ndugu zangu wamenitenga wakidai nimewaaibisha.
Siku ya tarehe 29 January mke wangu alichukua simu yangu na kuanza kupekua na mie huwa sina nongwa na huwa sifichi simu yangu siweki password yeyote sina tabia hizo sababu siwezi kufanya maujinga kwenye simu yangu.
Sasa shida imekuja mke wangu kakutana na sms ya mtu anayejifanya mganga na kiukweli Huyo mtu simjui na namba yake siifahamu kabisa ila sms yake inasomeka kama vile ananifahamu na tuliwahi kuonana ..sasa mke wangu kaanza vurugu na kunisema mimi mshirikina naenda kwa waganga ili nimroge atulie sijui simwamini na maneno kedekede kila nikijaribu kumweleza haelewi na ndugu wa mke na ndugu zangu wamepigiwa simu na kupewa malalamiko hayo kila nikijaribu kuwaelezea hawanielewi huku baadhi ya ndugu zangu wanadai nimewaaibisha ,
Wapo wanasema wanipeleke kwenye maombi nikaombewe binafsi nimekataa kila nikitaka kuwaelewesha hawataki kunielewa na siwezi kwenda kuombewa wakati ni sms ambayo binafsi sijui ni nani kaituma mpaka muda huu wamenitenga
Na hali ikiendelea hivi nimeamua kutoa maamuzi mazito juu ya familia yangu liwalo na liwe