Ninetengwa na familia ,mke kanikimbia kisa message ya ushirikina

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Nipo kwenye simanzi kubwa kwa takriban wiki 2 sasa familia ya mke imenitenga ,mke kanikimbia na baadhi ya ndugu zangu wamenitenga wakidai nimewaaibisha.

Siku ya tarehe 29 January mke wangu alichukua simu yangu na kuanza kupekua na mie huwa sina nongwa na huwa sifichi simu yangu siweki password yeyote sina tabia hizo sababu siwezi kufanya maujinga kwenye simu yangu.

Sasa shida imekuja mke wangu kakutana na sms ya mtu anayejifanya mganga na kiukweli Huyo mtu simjui na namba yake siifahamu kabisa ila sms yake inasomeka kama vile ananifahamu na tuliwahi kuonana ..sasa mke wangu kaanza vurugu na kunisema mimi mshirikina naenda kwa waganga ili nimroge atulie sijui simwamini na maneno kedekede kila nikijaribu kumweleza haelewi na ndugu wa mke na ndugu zangu wamepigiwa simu na kupewa malalamiko hayo kila nikijaribu kuwaelezea hawanielewi huku baadhi ya ndugu zangu wanadai nimewaaibisha ,


Wapo wanasema wanipeleke kwenye maombi nikaombewe binafsi nimekataa kila nikitaka kuwaelewesha hawataki kunielewa na siwezi kwenda kuombewa wakati ni sms ambayo binafsi sijui ni nani kaituma mpaka muda huu wamenitenga

Na hali ikiendelea hivi nimeamua kutoa maamuzi mazito juu ya familia yangu liwalo na liwe

 
Hayo ma SMS ya kijinga watu huwa wanayatuma tu , we tulia akikaa huko kwao akichoka atarudi, wala usichukue maamuz magumu, it is just a matter of time.
 
Mbona wengi huwa tunapokea na kukemea ni wapuuzi fulani tu wanawatega watu wawaibie BI DADA NAYE ANA YAKE KACHOKA MAJUKUMU...ATAPATIKANA MTU MZIMA MWENYE BUSARA KUMWAMBIA KUWA HIZO NIMSG ZA KAWAIDA SASA ...NENDA SHITAKI TCRA WATAKWAMBIA KUWA ITS NORMAL ISSUE NOW
 
Hii hata mimi nilishatumiwa mara nyingi.
 
Ukweli ht mi nimeshazipata zaidi ya 50 nami ni mtumishi wa Mungu. Anaowahadithia hawamwelezi Ukweli kwamba zipo tu mtandaoni? Na yeye siku akizipata mfululizo atakuelewa. We tulia acha kupanic
 
Kama ni kweli wana lao jambo hao sababu kama ni hizo msg mbona siku hizi zinatumwa sana tena sio mtu mmoja.

Pole sana ila liangalie kwa undani hilo swala sababu msg haiwezi kuwa chanzo cha yote hayo. Yaani mandishi tu ndio yazue seke seke lote hilo. Mmh.
 
Ongea na huyo mganga amforwadie na mkeo iwe ngoma droo
 
Huyo mkeo kufikiri unataka kumroga labda yeye ndie anafanyaga hivyo kwako..
Au anayake kizaidi kwa sababu hata humu maujumne hayo yameongelewa.. sasa natumaini wadau watakusaidia kusechi uzi wa hizo msg halafu waonyeshe ndugu zako wa karibu.

Mkeo muache atange labda hata anamchepuko au anayojaribu kwako anashindwa.. ana tabia mbaya kwasababu hakufikiria kuwa ni ya biashafa akajiweka yeye kizaidi.
 
Hizo SMS nafikiri 200 nimeshazipokea. MARA ya kwanza niliogopa kidogo. Ilihusiana na matambiko ya Magari ya biashara. Zilizofuata nilikuwa nawatukana kinoma.
 


Andika ukiwa umetulia haraka za nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…