Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Busara na msimamo ndio jambo la msingi sana kwa mwanadamu anayejitambua, kujiamini na kujipanga kwa kesho yake.
Ajali ya kisiasa aliyoipata Dr. Bashiru ni pigo kubwa kwake na kwa watu waliokuwa wanamuamini. Bashiru ametupwa nje ya ulingo wa utawala wa siasa za CCM na sasa anakwenda kutumika kama kitambaa cha kufutia vumbi cha watawala ndani ya Bunge. Legacy yake imefutwa ndani ya muda mfupi sana.
Dr. Bashiru ni msomi mzuri na mwalimu wa chuo kikuu. Kazi ya kufundisha ndio kazi aliyoipenda na kuifurahia zaidi katika maisha yake. Huu ndio wakati wake wa kurejea Chuo kikuu kufundisha.
Akutukanae huwa hakuchagulii tusi, CCM na serikali yake hawamuhitaji tena Bashiru na huenda hawakuwahi kumhitaji kabisa (ni Magufuli yeye mwenyewe ndio alimhitaji Bashiru), walichomfanyia Bashiru kinatosha, akiendelea kuwa mbishi na mkaidi kikubwa na kibaya zaidi kitafuata.
Njia bora kwa Bashiru kwa sasa ni kuwakwepa wabaya wake na kukaa kimya. Ubunge wa kupewa haiwezi kumfanya kukaa kimya, ni ubunge wa kitumwa, atapikiwa majungu na kuzushiwa kila mbaya na wanaCCM wenzake.
Majuto ni mjukuu.