Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Asiyejua alikotoka, hakika hawezi jua anakoenda!
Moja ya urithi ambao awamu ya tano ilituachia ni somo la hatma ya aliyekuwa akijitambulisha kuwa mwanaharakati binafsi wa Rais Magufuli, ndugu Musiba.
Nani hakumjua Musiba enzi za JPM? Musiba kwa matendo na maneno yake, ni kama alikuwa ndiye msemaji wa ikulu, msemaji wa serikali, katibu mwenezi wa CCM, n.k. Musiba alimtukana kila anayejisikia kumtukana, alimuonya kila anayejisikia kumuonya, na hakuna aliyethubutu kumkemea.
Wakati ukapita, Mwenyezi Mungu akamwita mja wake, JPM. Tukaanza kusikia mara Musiba anadaiwa 1 bilion TZSH kwa kumtukana Membe, mara online Tv zake hazipo tena mwisho hata CCM wamemkata!
Mara zote nimekuwa nikijaribu kusema uzoefu wangu na CCM. Siasa ya CCM haijawahi kuwa siasa ya harakati. Katika CCM uenzetu ndio kila kitu. Unaishije na wana CCM wenzako ndio inaamua utafika wapi? Infact huu ndio msingi haswa wa uwepo wa makundi na mitandao ndani ya CCM.
Watu waliofanikiwa na kudumu kwenye nafasi kubwa CCM hutawasikia wakimtukana mtu, wakimkashifu mtu wala kugombana na mtu. Mifano yao ni pamoja na Samia, Jakaya, Pinda, Mwinyi, Nchimbi, Lukuvi, Jenista, Simbachawene, Majaliwa, Mwinyi, na vijana kama Mavunde, Ndejembi, Ridhiwani, Aweso n.k
Akina Mchange, Kombo, Yona wa Chalinze na Sheikh Mwaipopo ni vyema wakawa waangalifu kama wana ndoto za kufika mbali kwenye siasa. Wenye hekima hujifunza kwa makosa ya wengine, lakini wapumbavu hujifunza kwa makosa yao wenyewe. Musiba ni case study nzuri sana